JIKE SHUPA MI’ SIYO SISTADUU, NANYONYESHA MWANZO MWISHO

Zena Abdallah ‘Jike Shupa’

MUUZA nyago kwenye video za wanamuziki mbalimbali Bongo, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ amefunguka kuwa atamnyonyesha mwanaye hadi mwisho kwani yeye siyo sistaduu.

 

Akichonga na Shusha Pumzi, Jike Shupa alisema kulikuwa na maneno mengi yaliyokuwa yakisemwa alipokuwa mjamzito kuwa hataweza kulea mtoto atakayemzaa, lakini sasa anafanya hivyo.

“Nataka kuwaonesha niko tofauti kabisa na wanavyonifikiria. Kwanza ninamnyonyesha mtoto wangu na nitamnyonyesha hadi mwenyewe asema mama inatosha, acha niende shule,” alisema Jike Shupa ambaye alijifungua mtoto wa kike hivi karibuni.


Loading...

Toa comment