The House of Favourite Newspapers

Jini Kabula, Lulu Diva Pachimbika

0

lulu divaLulu Abbasi ‘Lulu Diva’

Ubuyu: Hamida Hassan, Wikienda

 DAR ES SALAAM: Pamechimbika! Mwigizaji wa kitambo Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ na shostito wake kipenzi ambaye ni video queen maarufu, Lulu Abbasi ‘Lulu Diva’, wameingia kwenye bifu zito, kisa kikidaiwa ni penzi la mchezaji wa Simba (jina linahifadhiwa kwa sasa).

Ubuyu kutoka kwa sosi wa karibu wa mastaa hao ulieleza kwamba, kabla ya mambo kwenda mrama, Kabula na Lulu walikuwa marafiki wa kuvaliana hadi nguo na kila mmoja kulala kwa mwenzake lakini sasa wanasakana na kurushiana matusi.

“Hivi mnajua mjini kuna bifu jipya? Ni la Kabula na Lulu Diva, wamegombana na kutukanana vibaya mno.

Kabula (1)Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.

 “Kabula anamtuhumu Lulu Diva kuwa anatembea na mchezaji wa Simba ambaye Lulu Diva ndiye aliyewaunganisha hadi wakawa wapenzi,” alisema mnyetishaji wetu kwa ombi la kutotajwa gazetini.

‘Kikulacho’ huyo alifunguka kwamba, kuna rafiki wa karibu wa Kabula ndiye alimjaza upepo (maneno) Kabula bila kuchunguza vizuri kuwa Lulu Diva na mchezaji huyo ni

 ndugu kwani mrembo huyo amelelewa nyumbani kwa wazazi wa mchezaji huyo na wanatoka jiji moja la Tanga hivyo wanaheshimiana.

Baada ya habari hizo kutua kwenye meza ya Ubuyu Ulionyooka, mwanahabari wetu alimwendea hewani Kabula na kumuuliza sababu ya kugombana na Lulu ambapo awali alidai kwamba hamfahamu Lulu Diva lakini baadaye alifunguka kuwa

 hawezi kuwa na bifu na msanii ambaye hata akifa hawezi kutolewa rambirambi na Mheshimiwa Rais Magufuli kwa sababu hajulikani.

“Nakuomba sana tena sana, usiniandike na huyo mtu. Kama anatafuta kiki atafute na bwana’ke Nay wa Mitego (Msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki). Siwezi kuwa na bifu na yeye. Mimi nakuwa na bifu na wasanii wakubwa kama Wema (Sepetu) na (Irene) Uwoya,” alisema Kabula akiwa ‘amepaniki’.

LULU DIVA

Kabula alipoulizwa juu ya uhusiano wake na mchezaji huyo, alikana kumfahamu.

Alipotafutwa Lulu Diva, alifunguka mengi kuhusiana na sakata hilo akiweka wazi namna alivyoumizwa na Kabula kumsingizia kitu ambacho anakijua si cha kweli ambapo mahojiano yalikuwa hivi;

WIKIENDA: Lulu Diva kuna ubuyu hapa kuwa umegombana na shosti wako Jini Kabula kwa sababu ya mchezaji wa Simba, unalizungumziaje hili?

LULU DIVA: Dah! Duniani kuna maneno mengi, ukinyamaza watu wanafunguka tu na kwa kuwa limewafikia, mimi si wakuficha kitu.

WIKIENDA: Funguka ishu nzima ilivyo.

LULU DIVA: Kabula alikuwa rafiki yangu kipenzi. Mimi ndiye niliyemuunganisha kwa kaka yangu ambaye ni huyo mchezaji wa Simba, wakawa na uhusiano vizuri. Siku moja akajazwa maneno na rafiki yake (namuhifadhi jina) ila kuna siku nitamuweka wazi, nikashangaa ananitumia matusi ananiambia eti najifanya mchezaji huyo ni kaka yangu kumbe natembea naye.

“Nilisikitika sana lakini kutokana na yale matusi, niliamua kumjibu tukavunja urafiki.

WIKIENDA: Mchezaji huyo ni kaka yako kivipi?

LULU DIVA: Mama wa mchezaji huyo na mama yangu ni marafiki na ni kama ndugu. Mimi nililelewa kwa akina… (anataja jina la mchezaji huyo) huko Tanga na nilivyokuja Dar bado tuliendelea na ukaribu kama kaka na dada, ndiyo nikamuunganisha kwa Kabula akawa wifi yangu, huo ndiyo uhusiano wetu.

Baada ya wawili hao kufunguka, mwandishi alimwendea hewani mchezaji huyo kwa siku mbili mfululizo hakupokea simu na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa SMS hakuujibu. Wikienda linaendelea kumtafuta na litakapojiridhisha litaweka wazi ubuyu wake.

 

Leave A Reply