The House of Favourite Newspapers

Jini Mauti-27

0

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA Michael alining’ang’aniza lakini msimamo wangu ulikuwa uleule kwamba nisingeweza kuwa naye kwa sababu niliamini ilikuwa ni lazima siku moja tufanye mapenzi na baada ya hapo ambacho kingefuatia ni mauti tu.
Endelea…

Kila siku ilikuwa ni lazima Michael anifuate darasani kisha kunichombeza kwa maneno yake matamu kwa lengo la kukubali niwe naye lakini msimamo wangu haukulegea, bado niliendelea kuwa vilevile kwamba sikutaka kuwa naye.

Wakati Michael akiendelea kunifuatilia, naye Sifael alikuwa kwenye kasi ileile, kila siku alionekana kuwa mtu mwenye hasira mno kila alipomuona Michael akija na kukaa pale nilipokuwa. Alimchukia kwa kuwa alimpenda msichana ambaye hata naye alimpenda kwa mapenzi ya dhati.

Japokuwa alinipenda sana lakini Sifael alikuwa muoga, hakuwa tayari kunifuata na kuniambia ukweli kwamba alikuwa akinipenda ila kila nilipomwangalia niligundua alikuwa akinipenda sana.
Siku zikaendelea kukatika, niliendelea kuroga pasipo kujulikana, tulikesha sana makaburini tukiroga, hakukuwa na mtu aliyekuwa akitutisha zaidi ya wachungaji tu. Wakati mwingine tulikuwa tukienda mochwari, huko tulikuwa na kazi ya kuchukua viungo vya binadamu.

Baada ya siku kadhaa, kidato cha nne wakatarajia kufanya mahafali, walipanga kufanyia katika Ufukwe wa Coco. Ki ukweli sikutaka kwenda lakini Michael alinisisitiza kwamba nilitakiwa kwenda kwa ajili ya kumpa kampani, nikakubaliana naye.

Siku hiyo tulikusanyika kwa wingi sana, ilikuwa kama saa nane mchana hivi. Watu tulikula na kunywa na wengine kwenda kuogelea. Sikuwa sawa, nilikuwa na mawazo yangu tu kwani tangu kujiunga na kuwa mchawi, kwa kweli sikuona faida yoyote ila kujitoa lilikuwa suala gumu.
“Mbona upo hivyo?” aliniuliza Michael.
“Nipo vipi?”

“Hauna furaha! Tatizo nini?’
“Hakuna tatizo.”
“Kweli?”
“Ndiyo!”

Michael hakutaka kuniuliza maswali zaidi, alichokifanya ni kuondoka kuelekea katika uwanja wa kucheza na kuanza kucheza. Muda mwingi macho yake yalikuwa kwangu, alionekana kama mtu ambaye muda wote alitamani niwe namwangalia jinsi alivyocheza.

Ilipofika saa 12:30 jioni, tayari giza lilianza kuingia. Nilimwambia Michael kwamba nilitakiwa kuondoka lakini hakutaka kukubaliana nami, aliniambia kwamba tuendelee kukaa kwani kama kuondoka tungeondoka tu.

Sikuwa na sababu ya kukataa, tuliendelea mpaka ilipofika saa moja usiku. Tayari giza lilikuwa limeingia ndipo aliponiambia kwamba alichoka kucheza, hivyo alitaka twende kutembea.
“Wapi?”

“Kule kwenye mawemawe.”
“Ila si unaona giza!”
“Kwani unaogopa giza? Wewe twende tu, mlinzi wako nipo hapa,” aliniambia.
Nilijua nini kingetokea, nilijaribu kumwambia Michael kwamba sikutaka kwenda kule lakini akaning’ang’aniza sana, sikuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana naye.

Alionekana kubanwa, kuna kitu alitaka kukifanya, alitaka kufanya mapenzi na mimi kitu ambacho hakikuwa kikikubalika moyoni mwangu. Tulitembea ufukweni mpaka sehemu iliyokuwa na kilima fulani ambapo kulikuwa na miamba kadhaa.

Hakukuwa na mtu yeyote aliyetuona, tulichokifanya ni kusogea mbele ni sauti za mawimbi tu ndizo zilizokuwa zikisikika mahali hapo. Tukaelekea sehemu ya chini iliyokuwa na mwamba uliokuwa na uwazi mkubwa, akaniambia tukae hapo.

“Kuna nini?” nilimuuliza huku nikiwa na hofu.
“Davina…”
“Abeee.”
Akanisogelea zaidi, akausogeza uso wake karibu yangu, nikaanza kuzisikia pumzi zake nzito, akabaki akiniangalia tu kwa macho yaliyojaa matamanio. Hakuzungumza kitu, alichokifanya ni kuipandisha juu sketi yangu.

“Unataka kufanya nini?”
“Subiri kwanza.”
“Hapana Michael, siwezi kufanya hivyo,” nilisema huku nikijitahidi kumzuia.

“Unaogopa nini? Kuna nani anatuona? Mbona unakuwa hivyo? Davina, sisi ni wapenzi na si marafiki, wewe si dada yangu na mimi si kaka yako, tatizo lipo wapi?” aliuliza Michael.
“Michael! Sitaki ufe!”
“Nife? Nife kivipi?”

“Ukifanya mapenzi na mimi, utakufa.”
“Hahah! Sasa ajabu ipo wapi hapo? Kama kufa kila mtu atakufa,” aliniambia huku mikono yake ikifungua vifungo vya blauzi yangu.

Kwa kweli niliogopa, kichwa changu kilikumbuka matukio yaliyotokea, niliwakumbuka wanaume watatu waliokufa mara baada ya kufanya nao mapenzi hivyo nilijua hata kwa Michael ingetokea hivyo.
Nilimuonya kwamba hakutakiwa kufanya mapenzi na mimi kwa sababu angekufa lakini hakutaka kusikia hata kidogo, tena ndiyo kwanza aliniambia kama kufa kila mtu atakufa.

Sikupenda kuona Michael akifa, nilijitahidi kumzuia lakini ilishindikana kabisa, mwisho wa siku nakuja kushtuka, blauzi haikuwa mwilini mwangu na hata sketi ilitupwa chini na hivyo kuanza kufanya mapenzi nami huku akiwa amenilaza chini.

Sikusikia raha yoyote zaidi ya kulia kwa uchungu kwani niliamini ilikuwa ni lazima Michael afariki dunia palepale. Hivyo ndivyo ilivyotokea, nikahisi joto likianza kupanda mwilini mwake, alianza kutetemeka na mara nikamuona akianza kukakamaa.

Hakuchukua muda mrefu katika hali hiyo, mara nikayaona macho yake yakianza kubadilika rangi, yakaanza kuwa mekundu huku meno yake yakianza kugonganagongana, ndiyo alikuwa ameanza kuwa katika hali ya mwanzo ya kukata pumzi.

Niliogopa, nilitetemeka, nikamshika vilivyo Michael huku nikimuita, asiniache peke yangu, asife pale tulipokuwa. Aliendelea kuwa kwenye hali ileile, alikuwa chini, mapovu yakaanza kumtoka na mwili kuanza kubadilika rangi.

Niliogopa sana, sikutaka kubaki mahali hapo, nilichokifanya ni kuvaa haraka na kukimbia. Sikurudi kule walipokuwa wanafunzi, nilikimbia na kurudi nyumbani huku nikionekana kuchanganyikiwa.
*****
Kama kawaida yetu wachawi tulijazana katika uwanja wa kukutania, siku hiyo ilikuwa ni siku ya kusherehekea, siku ya kula nyama na kunywa damu tu. Kama kiongozi wa wachawi mahali hapo, kila mtu aliniheshimu, niliogopeka na kila mchawi niliyekuwa nikizungumza naye, alinioneshea heshima kubwa.

Nyama za binadamu zilikuwa mezani, hazikuwa zimepikwa, zilikuwa mbichi ambazo nyingine zilikuwa na damu.
Nililetewa bakuli kubwa lililojaa nyama nyingi, nilipoletewa, nikaliweka juu ya meza na kuanza kuchukua kipande kimoja baada ya kingine.

Je, kilifuatia nini? Usikose mwendelezo wa simulizi hii ya aina yake wiki ijayo.

Leave A Reply