The House of Favourite Newspapers

Jini Mauti-30

1

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA
“Kivipi?”
“Kwani haujaelewa?”
“Yaani ndiyo utakuwa mwisho wa mimi na wewe kuwa pamoja?”
Endelea…

“Nimesema mwisho wa mimi na wewe kuonana, yaani baada ya hapo, hautoniona tena,” aliniambia huku akiniangalia machoni.
Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nikagundua kwamba mboni za macho ya John hazikuwa zikicheza.
“John…” nilimuita.
“Unasemaje?”
“Wewe ni nani?”
“Kivipi tena?”
“Sikueleweelewi mpenzi,” nilimwambia.
“Hahaha! Eti mimi ni nani! Binadamu kama wewe.”
“Hapana! Unaonekana wa ajabu sana.”
“Najua. Ila mimi siyo jini, naomba usiogope,” aliniambia.
“Mmmh!”
“Tatizo nini? Mbona unakuwa na hofu.”
“Hakuna kitu.”
Hata nilipoagana naye nilikuwa na maswali mengi kichwani mwangu, nilibaki nikijiuliza kuhusu John lakini sikupata jibu. Usiku wa siku hiyo nilipokutana na wachawi wenzangu nikawaambia kwamba kulikuwa na sehemu tuliyotakiwa kwenda, ila tusingeweza kwenda wote, ilikuwa ni lazima tujigawe, yaani twende wachache, kama watatu hivi.

Nilitaka kujua ukweli juu ya John, alikuwa nani? Jini au binadamu. Baada ya kumaliza kikao tukaondoka na nyungo zetu mpaka alipokuwa akiishi John. Kama ilivyokuwa, tukapitia katika pembe ya nyumba na kuingia ndani.

John alikuwa amelala kitandani, nikamsogelea mahali pale na kumwangalia, nilikuwa nikimchunguza, wachawi wenzangu waliokuwa mle ndani wakaanza kuniangalia kwa mshangao.
Hawakuelewa sababu ya mimi kufanya vile, yaani kumchunguza sana John kama mtu niliyekuwa nikitafuta kitu fulani. John alikuwa binadamu wa kawaida, si jini kama nilivyohisi, sasa kwa nini mboni za macho yake hazikuwa zikicheza? Kila nilipojiuliza, nilikosa jibu, nilipomaliza tukaondoka zetu.

Bado maneno yake kwamba siku hiyo ingekuwa mwisho wa yeye kuonana nami yalinitia hofu, sikujua alimaanisha nini na kwa nini aliniambia maneno hayo tena katika kipindi kigumu kama hicho, nilibaki na mawazo hayo mpaka siku ambayo tulianza safari ya kwenda Bagamoyo.

Njiani, nikaanza kujiwa na mawazo juu ya mauti ambayo ingeweza kumkuta John baada ya kufanyanaye mapenzi, moyo wangu uliogopa lakini sikuwa na jinsi, nilitakiwa kukubaliana na hali iliyokuwepo kwamba iwe isiwe ni lazima nifanye mapenzi na John.

Tukaenda kwenye loji moja, ilikuwa ni ya gharama kidogo, John alilipia na kuingia ndani. Kila nilipokuwa nikimwangalia moyo wangu ulidunda sana, nilimpenda na nilifikiria kwamba huo ndiyo ungekuwa muda wangu wa mwisho kuonana na John kwani baada ya kufanya mapenzi, angefariki dunia.

Upole wa John ulikuwa mpaka chumbani, mimi ndiye niliyemsogelea na kuanza kumvua nguo zake, nilijitahidi kupitisha mikono yangu huku na kule, nikimshika hapa na pale ilimradi mwisho wa siku tufanye kile kilichotupeleka ndani ya chumba kile.

Nilimfanyia hivyo kwa dakika kumi, ikawa zamu yake ambapo akaanza kufanya vilevile. Ilichukua muda wa dakika thelathini, akaja kifuani kwangu na kuanza kufanya mchezo ule.

Nilishikwa na hofu, nikajua kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wa John, kilichonishangaza ni kwamba hakufa, aliendelea kushughulika nami kwa muda wa dakika arobaini na tano, alipomaliza, akasogea pembeni na kupumzika.
“Vipi?” nilimuuliza huku nikishangaa.
“Poa.”
“Upo salama?”
“Ndiyo! Kwani vipi?”
Kwa kweli nilishtuka mno, sikuamini kilichokuwa kimetokea, ilikuwaje John awe salama na wakati alitakiwa kufa kama ilivyokuwa kwa wanaume wengine, kila nilipojiuliza, nikakosa jibu. Hapo nikaanza kupata jibu kwamba inawezekana sikuwa na uwezo wa kuua tena, yaani mwanaume yeyote ambaye angefanya mapenzi nami, asingekufa kama ilivyokuwa zamani. Nikamshukuru Mungu katika hilo pasipo kujua kwamba huyu John alikuwa nani.
“Davina…” aliniita.
“Abeee…”
“Ni muda wa kuondoka.”
“Yeah! Ngoja nijiandae tuondoke.”
“Simaanishi kwenda Dar.”
“Kumbe kwenda wapi?”
“Si nilikwambia kwamba hatutoonana baada ya hapa?”
“Ndiyo!”
“Basi huu ndiyo muda.”
Aliniambia, akainuka kitandani, akaanza kuvaa nguo zake haraka, alipomaliza, akaanza kuufuata mlango. Akaushika na kuufungua na mimi nikamfuata, alipotoka nje na kuubamiza mlango, sekunde mbili tu nami nikaufungua, kilichonishtua, sikuweza kumuona John. Nikaogopa.
*****
Nilichanganyikiwa mno, sikujua ni kitu gani kilichotokea mpaka John kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Nilichokifanya ni kutoka nje, nikaanza kumtafuta John lakini sikuweza kumuona, kila nilipoangalia, palikuwa peupe.
Sikutaka kukaa Bagamoyo, siku hiyohiyo nikarudi nyumbani huku nikiwa na mawazo sana juu yake. Nilipofika nikajifungia chumbani na kuanza kufikiria juu ya kile kilichokuwa kimetokea Bagamoyo.

Bado nilijiuliza juu ya John, alikuwa nani. Jambo lililotokea lilinishangaza, kila nilichokuwa nikijiuliza nilikosa jibu kwani kichwa changu kilichanganyikiwa mno. Kwa sababu nilikuwa nimechoka sana, usiku wa siku hiyo sikwenda kuroga kama zilivyokuwa siku nyingine.

Asubuhi ilipofika nikaamka na kwenda shule. Nilipofika huko, sikutaka kuliweka wazi suala la John, nilibaki kimya kabisa. Macho yangu hayakutulia, nilidhani kwamba John angeweza kuibuka shuleni lakini sikufanikiwa kumuona.

Mpaka tunaingia darasani, nilipoangalia kiti chake, hakuwepo jambo lililowafanya wengi kuuliza alikuwa wapi lakini hakukuwa na aliyekuwa na majibu. John hakuwahi kutega shule, kila siku alifika shuleni, hakuwahi kuwa mgonjwa, kila siku alionekana kuwa mzima wa afya, sasa siku hiyo alikuwa wapi? Kila aliyejiuliza, alikosa jibu.

Hiyo ilikuwa siku ya kwanza, wengine walikuja kuniuliza, majibu yangu yalikuwa mawili tu, sikumuona kwa kipindi chote na sikujua alikuwa wapi.

Je, kilifuatia nini? Usikose mwendelezo wake wiki ijayo.

1 Comment
  1. Th0m says

    st0ry isiy0 na hitimish0 n mbaya

Leave A Reply