The House of Favourite Newspapers

JK Awapasha Wana-Yanga

0

RAIS mstaafu wa  Tanzania wa awamu ya nne   Jakaya Mrisho Kikwete   Juni 27, alikuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa Yanga kupitisha rasimu ya mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo aligeuka kivutio kwa hotuba na simulizi zake zilizojaa mzaha na masikhara.

 

Kikwete aligeuka kivutio kikubwa kwenye hotuba yake pamoja na kuikumbusha klabu yake pendwa maarufu kama ‘wananchi’ kufanya usajili mzuri  kwa wachezaji wenye  hadhi  pamoja na kuvumilia makocha, lakini hakuacha kuchomekea  imani za kishirikina katika timu hiyo miaka ya nyuma.

“wachezaji hawawezi kuja leo mnataka ubingwa, yaani kocha anakuja leo, katikati ya msimu mwingine, mwisho wa msimu mwingine halafu mnataka mabadikiko. Lazima tuwe na subra.”

 

“Hakikisheni makocha na wachezaji wanahudumiwa vizuri, wasiwe wanadai mishahara ya mechi mbili au tatu halafu ukiwapeleka kwenye mechi ngumu wakashindwa unasema wamekuhujumu, sasa wamekuhujumu vipi hujamlipa mishahara?

 

Mkutano  huo uliofanyika katika ukumbi wa DYCC uliyopo Temeke  na kufungiliwa rasmi saa 4:00 asubuhi ,ulikuwa na ajenda kadhaa zinazolenga kuijenga upya klabu, japo ile yenye nguvu ilikuwa kubariki mchakato wa  mabadiliko ya klabu kwenda kwenye mfumo wa  uwekezaji.

 

Pia wajumbe wa  mkutano mkuu walionekana kufurahishwa zaidi na uwakilishwaji  wa mpango wa ujenzi wa makazi  ya wachezaji na viwanja vya kuchezea kule Kigamboni.

Leave A Reply