Diamond Afunguka Kukosa Tuzo

MWANAMUZIKI wa Tanzania, Nassib Abdul maarufu Diamond Platnumz amekosa Tuzo ya BET usiku wa kuamkia leo Juni 28, lakini Watanzania walio wengi wameendelea kumpongeza kwa hatua hiyo.

Tuzo hiyo imekwenda kwa Burna Boy wa Nigeria katika Kipengele cha Mwanamuziki Bora wa Kimataifa

 

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Diamond ameandika; “Kupitia tuzo hii nimeona ni kiasi gani Watanzania tuna umoja, upendo na kuthamini vya kwetu…Nawashkuru sana kila mmoja wenu kwa upendo mkubwa mlionionesha…

 

“Ni faraja kuona Dunia inapotaja nchi zenye wanamuziki bora, Tanzania inatajwa, ni jambo la kumshukuru Mungu….Na naamini wakati mwingine tutaibeba…nitafarijika kesho na keshokutwa msanii mwingine pia akiwa katika jambo la kuwakilisha Taifa tumpe nguvu kama mlionipa…. sisi ni #SwahiliNation sisi ni Taifa la Waswahili…”

 


Toa comment