The House of Favourite Newspapers

JK; “Nimelemewa”, JPM; “Nitakukumbuka”, Makonda; “Hautosahaulika”

Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameeleza maumivu aliyonayo kufuatia kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba. Kupitia akaunti yake ya Instagram, Kikwete ameandika ujumbe maneno yafuatayo:

 

“Nimelemewa! Nakosa maneno ya kuelezea huzuni na majonzi niliyonayo kwa kifo cha Ruge Mutahaba.

“Taifa limepoteza kijana wake mahiri, mbunifu na mzalendo wa kweli. Nimepoteza rafiki, mshirika mwaminifu na mtu ambaye amenisaidia kwa mengi ktk uongozi wangu na hata baada ya kustaafu.

“Moyo wangu uko pamoja na wazazi wake, ndugu zake na familia yake katika kipindi hiki kigumu. Namuombea kwa Mola ampe Mapumziko Mema Peponi. Ameen. “

Comments are closed.