The House of Favourite Newspapers

Jokate kufungua Tawi la Yanga Kisarawe

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, kesho Jumamosi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tawi la Yanga Mlipo Tupo lililopo Kisarawe Mjini Wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

 

Jokate atazindua tawi hilo lenye wanachama zaidi ya 100 ambalo ndilo la kwanza kuzinduliwa wilayani Kisarawe.

Katibu mkuu wa tawi hilo, Abdallah Muga, amesema pamoja na uzinduzi wa tawi hilo, pia kutakuwa na zoezi la ugawaji wa kadi kwa wanachama na kusajili wanachama wapya.

 

Pia tawi hilo litamtunuku nishani ya uvumilivu Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kwa kuiongoza timu hiyo katika kipindi kigumu ambacho walikipitia msimu uliopita.

 

“Tumewaalika viongozi wa juu wa Yanga, lengo la kumpa kocha wetu nishani ya uvumilivu ni kutambua mchango wake wa uvumilivu msimu uliopita wakati timu yetu ikiwa katika hali mbaya kiuchumi,” alisema Muga

Comments are closed.