The House of Favourite Newspapers

JPM Ahudhuria Mkutano wa 20 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Liberat Mfumukeko na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) kuhudhuria Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha leo Ijumaa Februari 1, 2019.

 

Magufuli akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Mhe. Gaston Sindimo.

 

Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudani ya Kusini Mhe. Barnaba Marial Benjamin akiwa na Balozi wa Nchi hiyo nchini Mhe. Mariano Deng Ngor wakati alipowasili katika ukumbi huo.

 

Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame akilakiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Liberat Mfumukeko na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo.

 

Magufuli akiwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda.

 

Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta alipowasili.

 

Rais wa Uganda Mhe. Yowweri Kaguta Museveni akilakiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Liberat Mfumukeko na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo.

 

Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) wakihudhuria Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha leo Ijumaa Februari 1, 2019. Picha na IKULU.

Comments are closed.