The House of Favourite Newspapers

JPM Akabidhi Nyumba Mpya za Magereza Ukonga

0
Rais  John  Magufuli akiongea baada ya kufungua rasmi nyumba za askari Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam kwenye sherehe ya kukabidhi nyumba hizo lo Alhamisi Januari 23, 2020.

RAIS  John Magufuli amesikitishwa na kitendo cha viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutia saini makubaliano ya zabuni ya kununua vifaa vya zimamoto na uokoaji vyenye thamani ya Euro milioni 408.5 (sawa na zaidi ya shilingi trilioni 1) kutoka kampuni moja ya nchi za nje bila kufuata sheria.

Rais  Magufuli akikata utepe kufungua rasmi nyumba hizo. 

Ameyasema hayo leo tarehe 23 Januari, 2020 wakati wa sherehe za ufunguzi wa majengo 12 yenye makazi ya familia 172 za maafisa wa Magereza, Ukonga, Dar es Salaam.


Magufuli amesema ameshangazwa kuona viongozi hao wameingia makubaliano hayo ilhali zabuni hiyo haijapangwa kwenye bajeti wala kupitishwa na bunge, huku kukiwa na mazingira ya ukosefu wa uadilifu kutokana na aina ya vifaa vilivyotajwa katika zabuni hiyo na viongozi hao kusafirishwa kwenda nchi husika kwa kugharamiwa na kampuni waliyokubaliana kusambaza vifaa hivyo.

…Akipeana mikono na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Hassan Zungu..

 Magufuli amempongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, kwa kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa wake ili kuwajibika kwa dosari hiyo, na amewashangaa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola,  na Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye kutowajibika kwa dosari hiyo.

…Akikagua moja ya nyumba hizo. 


“Nakueleza Mheshimiwa Lugola na Kamishna Jenerali Andengenye, ninawashangaa kuwaona mpo hapa> Ninawapenda sana lakini huu ndio ukweli, sitaki kuwa mnafiki, shilingi Trilioni moja na kitu, mtu anasaini wakati sheria zote zinajulikana.  Mwenye mamlaka ya kukopa fedha ni Wizara ya Fedha peke yake.  Wanajua, ikiwa hivyo basi kila wizara itakopa,” amesisitiza rais.

 

…Akiwa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ndani ya mojawapo ya nyumba hizo.


Aidha, amesema maafisa wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliohusika kupitisha makubaliano hayo wakati Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi akiwa msibani (alipofiwa na mkewe),  na maafisa wengine wa Wizara ya Mambo ya Ndani waliohusika katika kashfa hii, wajitafakari.

…Akipata maelezo kuhusu nyumba hizo. 

Ujenzi wa majengo hayo umegharimu shilingi bilioni 13 ambapo awali  rais  aliagiza Jeshi la Magereza lipewe shilingi bilioni 10 lakini baada ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) waliokuwa wakifanya kazi hiyo.

Leave A Reply