The House of Favourite Newspapers

JPM Alivyopiga Kampeni ya Kishindo Dar na Kuwanadi Wagombea wa CCM

0
Dkt. JPM katika kampeni hiyo.

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye anagombea tena uraisi kwa awamu ya pili jana amepiga kampeni ya kishindo kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar.

Mkutano huo wa kampeni ulifurika umati mkubwa wa watu ambapo Dkt. JPM alitumia nafasi hiyo kuwakumbushia wananchi hao maendeleo ya kasi aliyoiletea nchi ndani ya kipindi kifupi na kuwaomba wamuongeze kipindi kingine ili afanye makubwa zaidi ya hayo.

Sehemu ya umati uliofurika kwenye kampeni hiyo.

JPM aliyataja baadhi ya mambo aliyoyafanya kama vile kuboresha huduma za afyam usafiri wa anga, elimu bure, barabara za kisasa mpaka mitaani.

Akizungumzia miundombinu ya barabara amesema anataka baada ya muda fulani katika jiji la Dar, barabara za vumbi ziwe za kutafutwa.

Vijana wakishangilia baada ya kusikia kuboreshwa kwa mikopo ya vyuo vikuu.

Mengine aliyoahidi kuyafanyia kazi katika kipindi chake kilichobaki ni pamoja na kuboresha mikopo kwa wanavyuo, kuimarisha biashara ya mtandaoni ili kuongeza idadi ya wafanyabiashara wakubwa na matajiri katika nchi.

Baadhi ya wagombea udiwani wakila kiapo cha kuwatumikia wananchi wakati wakiongozwa kiapo hicho na Dkt. JPM

Kinamama, vijana na walemavu wameahidiwa kuunganishwa katika mikopo inayotolewa kwenye Halmashauri mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Wasanii nao kilio cha muda mrefu JPM ameahidi kukifanyia kazi kwa kusimamia suala la hatimiliki na mengineyo.

HABARI/PICHA :NA  RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply