The House of Favourite Newspapers

JPM Amjulia Hali Askofu Mkuu Ruwa’ichi – MOI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana kwa furaha na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye anapatiwa matibabu katika Taasisi hiyo ya Mifupa Muhimbili (MOI) mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa Kichwa.

 

Rais Magufuli akiongoza sala ya kumuombea Askofu  Ruwa’ichi ambaye anapatiwa matibabu katika Taasisi hiyo ya Mifupa Muhimbili (MOI)

 

Askofu Ruwa’ichi akimshukuru Rais Magufuli ambaye alienda kumjulia hali. Wakwanza kulia ni Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, kushoto ni Padre Dkt. Alister Makubi Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam

 

Rais Magufuli akiwa na Askofu Nzigilwa (kulia), Padre Dkt. Alister Makubi kushoto, Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar wakifurahia jambo pamoja na Askofu Ruwa’ichi ambaye hali yake imezidi kuimarika mara baada ya kufanyiwa upasuaji katika taasisi hiyo ya MOI. PICHA NA IKULU

Comments are closed.