The House of Favourite Newspapers

Simanzi Kifo cha Mtoto wa Mabeyo, JPM Afika Kutoa Pole – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Ndugu Nelson Mabeyo mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo nyumbani kwao Msasani jijini Dar leo.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimpa pole Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo nyumbani kwake Msasani mara baada ya kufiwa na mtoto wake Nelson Mabeyo aliyepata ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiongoza sala pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo na familia yake wakimuombea marehemu Nelson Mabeyo ambaye alifariki kwa ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara.

 

 

Comments are closed.