The House of Favourite Newspapers

JPM ATOA NDEGE YA SERIKALI KUPELEKA MWILI WA RUGE BUKOBA

Rais Dkt Magufuli ametoa ndege ya Serikali kwa ajili ya kuusafirisha mwili wa marehemu Ruge Mutahaba na waombolezaji kwenda nyumbani kwao Bukoba kwa ajili ya maziko.

Hayo yameelezwa leo Machi 1, 2019 na Msemaji wa familia ya Mutahaba, Raymond wakati akizungumza na wanahabari nyumbani kwao, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Mwili wa Ruge unatarajiwa kuwasili leo kutoka Afrika Kusini, na utazikwa kijijini kwao Kiziru wilayani Bukoba, Machi 4, 2019.

Comments are closed.