The House of Favourite Newspapers

JPM Awasilisha Michango Ujenzi Msikiti Chamwino

0

RAIS  John Magufuli leo Jumatatu, Agosti 24, 2020, amewasilisha fedha za michango iliyotolewa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Chamwino mkoani Dodoma.

Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi Sheikh wa Wilaya ya Chamwino Sheikh Suleiman Abdallah Matitu sehemu ya pesa za michango kwa ajili ya ujenzi wa msikiti wa wilaya hiyo leo Jumatatu Agosti 24, 2020. Pesa hizo zimetokana na harambee aliyoendesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Imakulata Ikulu Chamwino mkoani DODOMA Jumapili iliyopita

Fedha hizo zimewasilishwa na Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike kwa Sheikh Mkuu wa Wilaya, Suleiman Abdallah Matitu, muda mfupi baada ya swala ya adhuhuri iliyofanyika katika msikiti uliopo hivi sasa.

 Sheikh wa Wilaya ya Chamwino Sheikh Suleiman Matitu akiongea na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa njia ya simu wakati wa hafla ndogo iliyofanyika leo Jumatatu Agosti 24, 2020  ya kupokea sehemu ya pesa za michango kwa ajili ya ujenzi wa msikiti wa wilaya hiyo zilizotokana na harambee aliyoendesha Rais Dkt. Magufuli wakati wa uzinduzi wa Kanisa la Parokia ya Bikira Maria ya IKULU Chamwino mkoani DODOMA Jumapili iliyopita

Pamoja na kukabidhi fedha hizo, Magufuli amewapongeza na kuwashukuru watu wote waliounga mkono na wanaoendelea kuunga mkono uchangiaji wa ujenzi wa msikiti mpya na wa kisasa wa Wilaya ya Chamwino.

Muonekano wa msikiti wa Chamwino mkoani Dodoma kama unavyoonekana. leo. Msikiti huo upo katika mpango wa kujengwa upya kwa pesa za michango iliyotokana na Harambee iliyoitishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa Kanisa la Parokia ya Bikira Maria ya IKULU Chamwino mkoani DODOMA Jumapili iliyopita

Amesema msikiti huo utajengwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na ujenzi wake utaanza wiki hii. Amesema watu mbalimbali wameguswa bila kujali madhehebu ya dini waliyonayo na kwamba hiyo ni udhibitisho wa umoja na mshikamano walionao Watanzania.

Leave A Reply