The House of Favourite Newspapers

JPM: Iringa Kuna Baridi, Lakini Jizuieni, Tupunguze Ukimwi – Video

Rais Dkt. John Magufuli amewasihi wakazi wa mkoa wa Iringa, kuchukua tahadhari kutokana na maambukizi ya ugonjwa hatari wa UKIMWI ili kupunguza vifo na vinavyosababisha kupungua kwa nguvu kazi ya taifa.

 

Rais Magufuli amesema hayo wakati akihutubia kwenye uzinduzi wa Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kilolo mkoani humo kutokana na ripoti zinazoonyesha kwamba Iringa ni mkoa wa pili kwa kuwa na watu wengi wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi huku Njombe ikishika nafasi ya kwanza.

 

“Ninafahamu Maambukizi ya Ukimwi bado ni tatizo kubwa kwa mikoa ya Njombe na Iringa, nilidhani sababu ya msingi ni baridi lakini sina uhakika, kwa kuwa imeletwa na Mwenyezi Mungu lazima tuhakikishe tunajikinga na kuchukua tahadhari ili tusiendelee kuangamia,” alisema Magufuli.

VIDEO: MSIKIE RAIS MAGUFULI AKIHUTUBIA

Comments are closed.