The House of Favourite Newspapers

JPM Katavi: Mafisadi Wameanza Kurudisha Fedha – Video

Rais John Magufuli akivuta utepe na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Isaack Kamwelwe,  kuashiria ufunguzi wa barabara ya Sumbawanga-Kanazi ya kilomita 76.6 iliyokamilika kwa kiwango cha lami.  Ni  katika sherehe zilizofanyika Kanazi mkoani Rukwa

RAIS  John Magufuli, leo Jumatano, Oktoba 9, 2019,  ameanza ziara ya siku tatu mkoani Katavi ambapo amefungua barabara ya Kanazi – Kizi – Kibaoni yenye urefu wa Kilomita 76.6.

 

Magufuli yupo katika ziara ya siku tisa katika mikoa ya Songwe, Rukwa na Katavia ambapo amewasili katika Uwanja wa Kibaoni wilayani Mlele mkoani Katavi na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo akiwa ameambatana na mkewe, Janeth Magufuli,  na mawaziri mbalimbali.

 

Akizungumza na wananchi, amewahakikishia wananchi wa Katavi kuwa miradi mingi  mkoani humo itatekelezwa kwani fedha zipo.

“Hela zipo.  Mafisadi wameanza kurudisha hela, kwa nini  tuache kujenga hapa?” amesema.

 

Pia ameagiza kuanzishwa kwa chuo cha utafiti wa kilimo mkoani humo  na kusema vijiji 920 yakiwemo mapori tengefu 12  na misitu ya hifadhi ifutwe, ikiwemo kumega hifadhi ili kusaidia wananchi kuendeleza kilimo wakati vijiji 60 vilivyokuwa na migogoro ya ardhi vikiachiwa na kuwa vijiji rasmi.

 

MSIKIE RAIS MAGUFULI

Comments are closed.