The House of Favourite Newspapers

JPM: Mmechoma Mahakama, Mtaijenga Wenyewe – Video

Rais wa Tanzania, John Magufuli amefungua jengo la mahakama katika mji wa Mlowo mkoani Songwe baada ya wananchi kumueleza kuwa licha ya ujenzi kukamilika bado halijaanza kufanya kazi.

 

Rais Magufuli yupo mkoani Songwe katika ziara ya siku tatu ya kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo.

 

Rais Magufuli amefungua jengo hilo la mahakama leo Ijumaa Oktoba 4, 2019 licha ya kuwa suala hilo halikuwa katika ratiba yake.

 

“Tafuteni kibao andikeni Rais Magufuli amefungua mahakama hii leo tarehe 4 mwezi wa 10. Mkuu wa Mkoa niwakilishe fuatilia mahakimu wananchi wanahitaji haki,” amesema kiongozi huyo wa nchi.

 

Awali wananchi wa eneo hilo wamesema licha ya kukamilika kwa ujenzi, mahakama hiyo bado haijaanza kufanya kazi.

Comments are closed.