The House of Favourite Newspapers

JPM: Mmefanya Upumbavu, Siogopi Kuwambia ni Wapumbavu – Video

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amewacharukia baadhi ya wananchi wa Masasi mkoani Mtwara kwa kuchoma Hospitali, gari la wagonjwa na ofisi ya ardhi.

 

Magufuli amesema; “Mmeniuzi sana, mkachoma ofisi ya ardhi, ambulance na hospitali ili wagonjwa wawe wanakufa, ni mambo ya ajabu sana. Masasi hawakutakiwa kujengewa hata hospitali, waliochoma ni wapumbavu, tunakusanaya pesa kwa Watanzania, ili tuwasaidie halafu mnafanya ya hovyo.

 

“Nilichaguliwa kuwa waziri na mzee Mkapa, aliyenifundisha kazi ya uwaziri ni Mama Anna Abdallah, walimu walionifundisha wote wametoka hapa Masasi. Najisikia aibu sana kwa haya mnayofanya.

 

“Kwa hili mtubu rohoni mwenu na kwa Mungu, ni upumbavu mlioufanya wala siogopi kuwaambia ni apumbavu. Najua waliowasaidia kuchoma ni watu wachache na sio wananchi wote wa Masasi. Najua wananchi wa Masasi ni wazuri na wachapa kazi, msikubali hao wachache wawaharibie.

 

“Hii barabara nitaijenga kwa lami, lakini msiichome. Nimewasamehe kwa majina yote matakatifu ya Yesu na Mtume Mohammed, mimi hapa ni nyumbani. Changamoto za maji na umeme tutazishughulikia. Hapa sitasubiri feasibility study kwa sababu tutachelewa.

 

“Leo nimekua mkali kutokana na mambo ambayo mnafanya, naomba msirudie tena kufanya hivyo. Watu wa Ushirika mjipange sawasawa, mtaishia jela, zao la korosho mhakikishe mnasimamia vizuri na hakuna mwananchi anayedhulumiwa, pesa za korosho zilizobaki mjipange zianze kulipwa jumanne, mkishindwa Bashe ‘nitakuchapa viboko’, kwa sababu wewe ni mwanangu,” amesema Rais Magufuli. 

 

AMESEMA RAIS MAGUFULI

Comments are closed.