The House of Favourite Newspapers

Juuko Astaafu

0

Aliyewahi kuwa Beki wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Juuko Murshid ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ akiwa na umri wa miaka 27.

Juuko ametangaza kuachana na ‘The Cranes’ kupitia barua yake aliyoiwasilisha kwenye Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), na sasa ataendelea na jukumu moja tu, la kuitumikia klabu yake Express FC ya Uganda.

Katika Barua hiyo Juuko ameandika: “Nimeitumikia nchi vya kutosha na ni wakati wa mimi kupumzika
“Haukuwa uamuzi rahisi lakini pamoja na familia yangu na uongozi wangu, tumefikiri na kuona ni uwamuzi sahihi. Ninawashukuru FUFA, wachezaji wenzangu na wadau wote wakati nilipokuwa na Uganda Cranes.

“Ninawatakia Uganda Cranes mafanikio mema, sasa akili yangu naielekeza katika klabu yangu ya Express FC” amesema Juuko.

Juuko amecheza michezo 39 akiwa na The Cranes na kufunga bao moja.

Leave A Reply