The House of Favourite Newspapers

Timu Yapata Ajali Zambia

0

Timu ya Quattro Kalumbila FC inayoshiriki Ligi daraja la kwanza nchini Zambia imepata ajali asubuhi ya leo January 13, 2022 baada ya basi lao kuacha njia na kuanguka katika barabara ya Kapiri-Kabwe wakiwa njiani kuelekea Livingstone kwaajili ya mchezo ujao dhidi ya Livingstone Pirates.

Chama cha Soka cha Zambia (FAZ) imethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema “Watu wawili wamejeruhiwa na hakuna kifo”.

Pia FAZ imeghairisha mchezo wa Daraja la Kwanza kati ya Livingstone Pirates na Quattro Kalumbila FC hadi tarehe itakayopagwa.

Leave A Reply