The House of Favourite Newspapers

Juventus, Atletico Zamuwinda Saka

0

KLABU za Juventus na Atletico Madrid zimeanza harakati za kutaka kumsajili beki kisiki wa Arsenal, Bukayo Saka. Saka alionyesha kiwango cha juu kwenye michuano ya Kombe la Euro mwaka huu lakini mwanzoni mwa msimu huu bado hajawa kwenye makali yake.

 

Kinda huyo mwenye miaka 20, amekuwa akitajwa kuwa mmoja kati ya mabeki mahiri wa umri wake. Hata hivyo, Arsenal wameshasema kuwa hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo kwa kitita cha chini ya pauni milioni 43.

 

Juventus ndiyo walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kumpata mchezaji huyo lakini sasa Atletico Madrid wanaonekana kwenda kwa kasi kubwa.

 

Hata hivyo, kocha wa Arsenal Mikel Arteta amekuwa akisema kuwa hana mpango wa kumuuza beki huyo ambaye pia anaweza kucheza kama winga. Saka msimu huu tayari ameshaitumikia Arsenal kwenye michezo mitano akiwa bado hajafunga bao lolote kwenye ligi.

LONDON, England

Leave A Reply