The House of Favourite Newspapers

Jux ni Mzee wa Old Skuli

0

Msanii wa Bongo Fleva, Juma Jux, anasema yeye huwa anapenda kusikiliza nyimbo za zamani zaidi tofauti na anavyosiki­liza mikwaju ya wasanii ambao hawana muda mrefu kwenye gemu.

 

Jux amesema anapenda zaidi kusikiliza nyimbo za zamani na wasanii wa zamani kwa kuwa kule kuna muziki wa kweli tofauti na nyimbo za sasa ambazo zinaimbwa na wasanii chipukizi.

 

“Mimi sisikilizagi sana nyimbo, ila nyimbo ninazosikilizaga ni za zamani sana, nyimbo za wasanii wapya huwa sisikilizagi sana,” alisema.

 

Jux ambaye anamiliki brand na duka la mavazi la African Boy, kwa sasa ana muziki mpya unaoitwa I Love You akiwa na Gyakie.

Leave A Reply