The House of Favourite Newspapers

GSM Yajitoa Udhamini Ligi Kuu, TFF, Bodi ya Ligi Watajwa

0

Mdhamini Mwenza wa ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier Leagueq) 2021/2022 wamejitoa kuendelea kudhamini Ligi Kuu inayoendelea hivi sasa kuanzia leo Februari 7, 2022.

 

GSM waliingia Mkataba wa Miaka miwili na TFF wenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.1, Novemba 23, 2021.

 

Akizungumzia chanzo hasa cha kufikia uamuzi huo, Afisa Biashara Mkuu wa GSM Allan Chonjo amesema kwa ufpi ni kutotekelezwa kwa yale ambayo walikubaliana baina ya GSM na TFF.

 

Aidha, Mmiliki wa Makampuni ya GSM, Ghalib Said Mohammed (GSM) amejiuzulu nafasi yake ya Uenyekiti na mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).

Leave A Reply