The House of Favourite Newspapers

Jygga Lo: “Nilikuwa Simjui Jay Z Ni Nani Na Sikupenda Kufananishwa Nae”- (Video)

Ramadhan Ally maarufu kama Jygga Lo

Kama vile Harmo Rapa afananishwavyo na Harmonize msanii kutoka label ya WCB Wasafi ndivyo ambavyo Ramadhan Ally anafananishwa na rapa tajiri kwenye game ya Hip Hop duniani Shawn ‘Jay Z’ Carter.

Ramadhan Ally maarufu kama Jygga Lo ni Mtanzania anayefanya Hip Hop lakini kujulikana kwake kumekuja sio kwa muziki wake bali kwa kufanana kwake na rapa maarufu wa muziki huo duniani Jay Z 

 “kufananishwa mimi na Jay Z kulianza toka nipo darasa la tano, sita… lakini kipindi hicho nilikuwa sijui maana ya Jay Z ni nini, nilihisi pengine ni HB fulani hivi… “ Jygga Lo Alizungumza na wanahabari.

Akizungumza na wanahabari, Jygga Lo alifunguka na haya ya kusema…

Nilivyokuja kugundua Jay Z ni nani ilikuwa mwaka 2003, dada yangu alikuwa anaangalia TV na ulipigwa wimbo wa Jay Z unaoitwa ‘Excuse Me Miss’ nilivyokuwa naanza kula kijiko cha kwanza, dada yangu akaniambia ‘ebana eeh, unajua umefanana sana na huyu mkaka!’ Akaitaja ile Jay Z ndio ikabidi sasa nimwangalie maana nilijua Jay Z ni HB fulani, nilivyosogea kumuangalia vizuri nakumbuka nilichukia sana, sikutegemea kuwa nafananishwa na mtu kama yule…” 

Itazame interview nzima ya Jygga Lo na Wanahabari  hapa

Lakini Jygga Lo ana wimbo wake ‘Ex-Girlfriend’ hewani pia, kama bado hujakutana nao bonyeza play hapa chini uitazame.

Imeandikwa Na: Sandra Brown

Comments are closed.