The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Godbless Lema Aachiwa kwa Dhamana

Joseph Ngilisho, Arusha: MAHAKAMA Kuu Kanda ya Arusha, imemuachia huru Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbles Lema (CHADEMA) kwa dhamana ya shilingi milioni moja pamoja na wadhamini wawili wenye vitambulisho vinavyotambulika na serikali.

Mbunge Lema aliyesota mahabusu kwa takribani miezi minne akikabiliwa na kesi ya uchochezi, katika Gereza Kuu la Arusha lililopo Kisongo, hatimaye amepata dhamani na kupokewa kwa mbwembe na washabiki wake waliomtandikia kanga ili apite wakati akitoka mahakamani hapo.

Akisoma hukumu ndogo ya mbunge Lema katika mahakama kuu Arusha, jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Fatuma Magimbi alisema kuwa mbunge lema hakupaswa kukaa mahabusu muda mrefu kwani ilipaswa kupewa dhamana.

Akizungumza nje ya mahakama hiyo, Lema alisema kuwa Jamhuri ilikuwa na nia ya kumfunga lakini Mungu amempigania mpaka kutoka huku akimshukuru mke wake kwa jinsi alivyomfariji kwa kipindi akiwa anashikiliwa.

Alisema kuwa kwa sasa ameandaa waraka wa kumwandikia raisi kuwa wapo watu wanaoteseka bila kuwa na hatia magereza na kwamba atautoa hivi karibuni

Nae wakili mtetezi wa mbunge Lema, Peter Kibatala alisema kuwa mahakama kuu imelekeza kuwa mahakama za chini zisimamie madaraka yake na mamlaka yake bila kuyaachia na hivyo kwa sasa wanatakiwa kujiandaa kwa ajili ya kupambana na kesi.

Nae mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe alisema kuwa wanamkaribisha tena Lema bungeni na kwamba kamati ya chama imemaliza vikao vyake mjini hapa na kuwashukuru wabunge wa mikoa mbali mbali waliofika kutetea dhamana ya lema.

Aidha Mbowe amelaani vikali kitendo cha jeshi la polisi kutumia mamlaka yao vibaya kwa kuwapiga wananchi bila makosa kwa madai kuwa wanakuja kuleta vurugu huku lengo ni kuja kusikiliza mbunge wao.

Alisema kuwa kutokana na tukio hilo atampigia kamanda wa jeshi la polisi pamoja na mkuu wa upelelezi mkoa   kumweleza jambo hilo kuwa raia wana haki ya kuja kusikiliza kesi kwani wananchi wana haki yamkija kusikiliza kesi ya mbunge wao.

Amedai kuwa uonevu huo wataenda kuuzungumzia bungeni juu ya maswala ya jeshi la polisi kuwaoiga wananchi virungu.

 

Comments are closed.