The House of Favourite Newspapers

Kabila Linalohusudu Vitambi, Linalotembea Utupu-8

0
Tamaduni za mabinti wa Kabila la Bodi.

 

TUNAENDELEA kuwaletea simulizi ya kabila moja la nchini Ethiopia ambalo wavulana hushindanishwa kuotesha vitambi, hawa watu wanaohusudu vitambi na wa Kabila la Bodi wana vituko vingi vya ajabu. Vijana wote wa kiume waliobalehe hupewa mafunzo mbalimbali na wazee wao.

Mafunzo hayo ni kwa ajili ya kuwafanya jasiri pindi wakikutana na wezi wa mifugo yao au wanyama wakali msituni kama vile simba na chui.

 

Tamaduni za mabinti wa Kabila la Bodi.

 

Leo tunamalizia makala haya kwa kuangazia upande wa wasichana wanapobalehe. Hawa huchukuliwa kuwa ni watu wa kipekee na huheshimika na jamii kwa kuwa wanaonekana ni watu waliovuka hatua moja kwenda nyingine.

Wasichana wa Kabila la Bodi wanapobalehe kwanza kwa siku za mwanzo huwekwa ndani kwa wiki tatu ambapo hupewa mafunzo maalum na kuambiwa wazi kwamba sasa wamekua.

 

 

Tamaduni za mabinti wa Kabila la Bodi.

 

Shughuli hiyo huku kwetu huitwa unyago, hupewa mafunzo na wanawake maalum wenye umri mkubwa. Hufundishwa usafi na jinsi ya kuishi katika hali hiyo ya kuvunja ungo.

Hufungwa shingoni njuga na kila atakapopita watu watajua kwamba anayepita ni mwali aliyevunja ungo hivi karibuni. Imeelezwa kwamba hiyo hufanywa ili kwanza, kumpa heshima msichana huyo lakini pili ili wavulana waliofikia umri wa kuoa nao wamuone na kufanya chaguo lao kama kuna anayetaka kumuoa.

 

 

Tamaduni za mabinti wa Kabila la Bodi.

 

Wakiwa ndani kipindi cha unyago baada ya balehe wapo wanaopambwa miili yao kwa kuchanjwachanjwa au enzi za zamani kutobolewa mdomo wa chini na masikio na kuwekwa kibanzi ambacho huwa kwao ni moja ya mapambo kwa msichana. Hata hivyo, siku hizi wengi wameacha utamaduni huu.

Wasichana hao waliobalehe wengine hupambwa kwa kutengenezewa shanga nyingi na kuvishwa shingoni, hivyo kuonekana kuwa ni msichana wa kipekee anapopita mitaani.

 

Mama Kabila la Bodi na mwanaye.

 

 

Wengine hunyolewa nywele zao kwa mitindo mbalimbali ambayo ataichagua au kuchaguliwa na wale wanaowasimamia wakiwa kwenye ‘jando’ unyagoni.

Wapo wanaonyolewa kiduku, wengine hunyolewa miduara, wengine husukwa nywele zao kwa kuunganishwa na kamba maalum ambazo hupakwa rangi nyekundu na huvutia, hivyo kumfanya msichana kuonekana kuwa ni wa kipekee.

Hufundishwa kuwa makini na wavulana kwa sababu wakitembea nao kabla ya kuwaoa wanaweza kupewa mimba na kuwafanya wasiwe na heshima kwa jamii yao hasa wazazi.

 

Mama Kabila la Bodi na mwanaye.

 

 

Kwa Kabila la Bodi, msichana akizaa kabla ya kuolewa hukosa heshima kwenye jamii yake na huonekana kama vile ameleta balaa katika ukoo na kudhalilisha wazazi ambao huonekana hawakutimiza majukumu yao ya kuhakikisha msichana anajitunza na kupata mume wa kufunga naye ndoa.

Wavulana ambao huwanyemelea wasichana hao, wakikamatwa hutozwa faini bila kujali kama wamewapa mimba au la kwa sababu tabia ya uzinzi hupigwa vita na jamii hii, na ndiyo maana wasichana na wavulana wengi wana nidhamu ya hali ya juu.

 

Binti wa Kabila la Bodi.

 

Hufundishwa jinsi ya kumhudumia mume iwapo wataolewa na jinsi ya kutunza familia kwa kukamua ng’ombe, kusaga nafaka kwa kutumia mawe na mafundisho mengine yanayohusu unyumba pindi watakapoolewa.

Hufundishwa nidhamu kwa waume zao watakapoolewa na kutii pia kuwaheshimu wakwe zao lakini pia hufundishwa jinsi ya kulea watoto wao wakibahatika kuwapata.

NA MWANDISHI WETU NA MITANDAO

Leave A Reply