The House of Favourite Newspapers

Video: Mkazi wa Kimara Afunguka Kubomolewa Ghorofa ya Milioni 900

0
Mkazi wa Kimara Stop Over, Dar es Salaam, Nicomed Leo.

MKAZI wa Kimara Stop-Over, Dar es Salaam, Nicomed Leo (61) amefunguka juu ya kubomolewa nyumba yake ya ghorofa aliyosema ina thamani ya milioni 900 na ambayo sasa imewekwa alama ya X kwa ajili ya kubomolewa ili kupisha upanuzi wa Barabara ya Morogoro.

 

Nyumba hiyo, kwa mujibu wa Leo, ilikuwa na wapangaji waliokuwa wanamlipa zaidi ya Sh. milioni 10 kwa mwaka na kwa sasa wapangaji hao wameondoka kwenye nyumba hiyo baada ya kuwekewa alama hiyo na kudai kiasi walichokuwa wamekilipa kulingana na mkataba.

 

Aliendelea kwamba kwa vile alishindwa kuwalipa fedha hiyo, wapangaji hao waling’oa milango na kuondoka nayo.

Kujua mkasa mzima usikose mahojiano yatakayorushwa live muda mfupi ujao kupitia Global TV Online .

Kuangalia Subscribe hapa www.youtube.com/user/uwazi1

Leave A Reply