The House of Favourite Newspapers

Kadinda Ataja Sababu Za Zutoonekana Na Mademu

martin-kadinda-1     Mwanamitindo, Martin Kadinda.

Habari na Imelda mtema

Unapowazungumzia wanamitindo wakubwa Bongo, huwezi kuacha kumtaja Martin Kadinda. Licha ya kupata umaarufu kupitia kazi yake, Kadinda aling’ara zaidi alipoanza kumsimamia supastaa mkubwa Bongo, Wema Sepetu akiwa meneja wake.

Kazi yake ya uanamitindo imempatia tuzo kibao zikiwemo Mwanamitindo Bora Afrika Mashariki 2015, Mbunifu Bora wa Mavazi ya Kiume Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo na nyingine nyingi.

martin-kadinda-5

Meneja wa Wema Isaac Sepetu, Martin Kadinda akiwa na na Staa huyo.

Juzikati alipiga stori na gazeti hili na kufunguka mambo kibao kuhusu maisha yake na kueleza sababu inayomfanya asipende kuonekana na mademu. Shuka nayo:

Amani: Mambo vipi Kadinda! Unaweza kumwambia msomaji umaarufu wako umetokana na nini?

Amani:  Umaarufu wako ulitokana na nini?

 Kadinda: Ulitokana na  na kazi yangu ya ubunifu wa mavazi ndio chanzo cha umaarufu wangu.

martin-kadinda-9Martin Kadinda akiwa katika pozi.

Amani: Kuna ukweli wowote kuwa jina lako lisingekuwa kubwa kama usingekuwa meneja wa Wema?

Kadinda: Ukubwa wa jina langu umetokana na kazi zangu ila kwa kiasi kikubwa ni kwa watu maarufu niliowavalisha wamenisaidai sana mimi kufahamika  na pia moja malengo yangu ya kummeneji wema ni kuongeza wigo katika biashara zangu na kiukweli amenisaidia sana ninamshukuru siku zote kwa hilo kila wakati.

wema-sepetu-na-martin-kadinda3Wakifanya yao Wema na Kadinda.

Amani: Changamoto gani unakutana nazo kama meneja wa staa mkubwa Bongo?

Kadinda:  Unapokuwa una hela unaishia kufanya kazi kutokana na  kile anachotaka  mhusika pia ni ngumu sana kumsimamia mtu ambaye ana malezi tofauti  na uliyolelewa wewe hivyo inakuchukua  muda sana kuelewana na kuendana njia moja  na pia binadamu tunaishi kutokana na kile tunachokiamini hivyo changamoto za watu wanaotuzunguka  na utofauti wa ndoto ndio changamoto zenyewe.

martin-kadinda-3Martin  akicheka baada ya kuangalia kitu kilicho mbele yake.

Amani: Kipindi cha Wema yupo na aliyekuwa kigogo wa Ikula  Ck, vilizuka vitu vingi sana kuwa uliweza kujenga nyumba kwa kutumia hela zake wakati yeye hana nyumba unazungumziaje hilo?

Kadinda: Naomba nirekebishe kauli za watu mimi  sina  nyumba nina kibanda ambacho nimejenga kwa nyuma ya nyumba yetu  familia hivyo huwa napaita banda la uani na hata hivyo nimejenga kipindi cha  ‘ Single Buttons’ na n ilikuwa sijaanza kufanya kazi na Wema kama meneja wake.

Amani: Sasa kama wewe meneja  wake kwanini kwa kipindi chote hujaweza kusimamia kuwa na nyumba yake mwenyewe?

Kadinda:  Unajua suala la nyumba kwa Wema kutokuwa nayo mpaka sasa ni aina ya nyumba anayotaka kujenga  inahitaji hela nyingi sana  lakini kwa vile tayari ana miliki kiwanja  hivi karibuni watu wataiona  hiyo nyumba ninayoongelea.

Amani: Ni mafanikio gani umeyapata mpaka sasa hivi kupitia unamitindo?

martin-kadinda-7Kadinda: Kwa kweli sijafika sehemu ambayo naweza kusema nina mafanikio ila kikubwa nimeweza kuitangaza nchi yangu kupitia sanaa yangu hiyo na pia kuwa na mahusiano mazuri na wabunifu wakubwa  toka  nchi mbalimbali duniani na nimeweza kutembea sehemu tofauti.

Amani: Unazungumziaje watu kusema kuwa husimamii kazi za Wema ipasavyo  kwa maana anafanya vitu vingine ambavyo sivyo?

Kadinda:  Wema sio mtoto mdogo mimi napaswa kumshauri tu na kumuonesha njia  suala  la yeye kutofuata  ninachomueleza  ni maamuzi yake binafsi  na pia ikumbukwe pia nafasi ya kummeneji Wema sio kwamba natembea nayo kama kuna mtu anahisi anaweza kufanya hivyo anakaribishwa.

Amani: Vipi kuhusu harusi yako maana ilivuma baadae ikapotea   na vipi kuhusu mchumba wako huyo?

Kadinda: ( kicheko) Hilo watu walizusha tu ,muda w akuoa mimi ukifiuka tu wataona picha tu kwetu suala la ndoa ni la kifamilia tu zaidi hao wengine wataishia tu kulike picha kwenye mitandao ya kijamii.

Amani: Kuna video ilivuma hivi karibuni ikimuonyesha Wema na mwanamitindo Calisah wakiwa kwenye picha tata unalizungumziaje hilo kama meneja?

martin-kadinda-6Akiwaza jambo.

Kadinda: Mimi sijaiona  nimesikia tu na hata kama ningekuwa nimeona nadhani Wema, Wema peke yake ndio anapaswa kutoa majibu ya kuhusu video hiyo maana ni maisha yake halisi.

Amani: Baada ya kutoa nguo yako aina ya Kwachukwachu unejipanga na kitu gani kingine?

Kadinda: Inachukua miaka miwili kuja na vazi jipya  kwahiyo tukutane 2017.

Amani:  Nakumbuka kama kipindi cha nyuma ulishawahi kuwa meneja wa Lulu ni sahihi?

Kadinda: Hapana Lulu ni mtu wangu wa karibu tangu tupo shule ni kama mdogo wangu  na tunashauriana vitu mbalimbali.

Amani : Hivi karibuni  ilidaiwa mlikuwa kwenye mgogoro mzito na Wema mpaka hamkuwa mnazungumza vipi kuhusu hilo,na pia hujafikiria kuwakalisha pamoja Muna na Wema wakamaliz atofauti zao?

Kadinda: Migogoro yangu na Wema inatokea mara nyingi tu kwa hiyo ni kawaida kwetu kuhusu Muna na Wema sio mimi niliwakutanisha mwanzo kwenye urafiki wao  hivyo watapatana wenyewe tu kwasababu migogoro kwa marafiki ipo tu.

Amani: Kama meneja Wema alishakuwa na marafiki kama Kajala, Wema, Snura na Aunt ungependa kati ya hawa ni yupi angekuwa lakini wa kudumu kwake.

Kadinda:  Mimi ningemshauri dada zake au mama yake lakini pia  unajua urafiki ni swala la mtu binafsi siwezi kusema yupi anamfaa, pia ili Wema aweze kufanikiwa zaidi anapaswa kufanya kazi zake mwenyewe.

Amani: Wanawake wengi wanakusema kuwa unaringa kwasababu hata ukiwaona wazuri huwatongozi japokuwa hujawahi kuonekana na mwanamke?

Kadinda:  Naheshimu mwanamke hasa kwa kuwa  naamini sio kila mwanamke nitakayekuwa  nae kwa mahusiano  ndo nitakayemuoa na hiyo kwasababu nina binti yangu mdogo sitaki akue akiona habari zangu za mahusiano sio malezi ninayomlea ndio maana  familia yangu na mahusiano yangu nayaweka mbali na media.

Amani: Kama meneja ungetamani Wema  awe na nafasi gani katika jamii?

Kadinda: Kila anayempenda Wema,anataka kuona akiwa na nyota inayong’aa Tanzania na Afrika nzima kwa ujumla hilo ndio ombi langu kwake tu.

Amani: Kuna ugomvi ulitokea kati ya wewe na mama Wema kwa madai kuwa ulipewa hela ya kumnunulia Wema kiwanja ukanunua kisichokuwa na hadi ya pesa uliyopewa vipi hilo?

Kadinda:  Sijawahi kuigombana na mama Wema hayo ni maneno  tu nagombanaje na mama sasa? Siwezi ni maneno tu.

Amani: Kumbe una mtoto nilikuwa sijui

Kadinda: ndio nina binti wa miaka nane sasa nilimpata nikiwa shule.

Amani: Nakushukuru sana Kadida kwa ushirikiano wako?

Kadinda: Asante sana.

 

Comments are closed.