The House of Favourite Newspapers

Kagere: Nitawafunga Tena Yanga Uwanja wa Taifa

0

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere raia wa Rwanda, amesema atawafunga tena Yanga katika mchezo wa leo Jumapili wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Kagere ametoa kauli hiyo baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa uwanjani hapo Januari 4, mwaka huu kufunga bao moja katika sare ya 2-2. “Kwanza naamini mchezo utakuwa mgumu kwa sababu Simba na Yanga zinapocheza presha inakuwa kubwa kwa kila upande kuhitaji ushindi.

 

“Kitu cha msingi tunachokiangalia ni kushinda, mimi nikiwa mmoja kati ya wenye malengo ya kuifunga tena Yanga kwani ndiyo kazi nyangu, hivyo nitapambana kwa nguvu zangu zote kuhakisha nafunga, najua haitokuwa rahisi lakini nataka kuona nawafunga tena,” alisema Kagere.

Leave A Reply