The House of Favourite Newspapers

Kagere: Tukija Bongo, tunarudi kwa kishindo

MSHAMBULIAJI machachari wa Simba, Meddie Kagere raia wa Rwanda ameweka bayana kwamba kwa sasa hawana habari na Ligi Kuu Bara kwa sababu wana mechi za kimataifa lakini siku ambayo wataanza kucheza mechi za ligi hiyo watarudi kwa kishindo.

 

Kagere ambaye alikuwa Gor Mahia ya Kenya kabla ya kutua Simba jana Jumamosi alikuwa mmoja wa washambuliaji wa timu hiyo ambao walicheza mechi ya kimataifa dhidi ya Al Ahly.

 

Straika huyo aliyefunga mabao saba katika Ligi ya Bara ameliambia Spoti Xtra, kwamba kwa sasa wala hawashtushwi na matokeo ya wapinzani wao wanayoyapata kwani siku ambayo watarudi watafanya kweli kwa kupata pointi kwenye kila mechi yao.

 

“Hatuna mawazo na ligi kuu hata kidogo kwa sababu sasa tumekuwa tukicheza mechi nyingi za kimataifa, hivyo hatuwezi kufikiria juu ya mechi mbilimbili.

“Tunachokifanya ni kumaliza mechi zetu hizi za mabingwa kisha ndiyo tugeukie huku. Ninaamini kwamba tukianza kucheza mechi za ligi basi tutakuwa na moto wa hali ya juu kwa sababu tunataka kupata pointi katika mechi zote ambazo tutacheza,” alisema Kagere.

Comments are closed.