The House of Favourite Newspapers

Kaizer Chiefs Yaipa Straika Yanga

0

YANGA ishindwe yenyewe! Ndiyo utakavyoweza kusema ni baada ya Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kutangaza kuachana na straika Mzambia, Lazarous Kambole.

 

Katika msimu uliopita, Yanga ilikuwepo katika mipango ya kumsajili Mzambia huyo kabla Chiefs kuingilia kati na kumnasa kwa dau la dola 200,000 (zaidi ya Sh 459m) akitokea Zesco United.

 

Yanga hivi sasa ipo kwenye mipango ya kukisuka kikosi chake ikiwemo safu ya ushambuliaji ambayo imeshindwa kuonyesha makali inayoongozwa na Mghana Michael Sarpong na Fiston Abdoulrazack.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, kutoka Chiefs upo uwezekano mkubwa wa mshambuliaji huyo kuachwa katika mipango ya klabu hiyo baada ya kufanya vibaya katika ligi.

 

Chiefs itaachana na nyota huyo kwa lengo la kuacha nafasi ya kumsajili mshambuliaji mwingine mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao zaidi ya Kambole ambaye hana nafasi ya kudumu ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

 

Klabu hiyo iliyofuzu Hatua ya Robo ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwaondoa wapinzani wa Yanga, Simba kwa kuwafunga mabao 4-3.

 

Yanga ina nafasi kumnasa mshambuliaji huyo kutokana na husiano mazuri yaliyokuwepo hivi sasa mdhamini wa klabu hiyo, Kampuni ya GSM.

 

Yanga kwa kupitia Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili, Injinia Hersi Said, hivi karibuni alitembelea Klabu ya Chiefs kwa ajili ya kujenga uhusiano kati ya klabu hizo mbili.

 

Yanga kwa kupitia Mshauri wa klabu hiyo, Senzo Mazingisa, hivi karibuni alisema: “Uongozi umepanga kufanya vitu vyake kwa usiri mkubwa tofauti na misimu miwili iliyopita, lengo ni kufanya usajili utakaokuwa bora na kisasa.”

STORI: WILBERT MOLANDI

Leave A Reply