The House of Favourite Newspapers

Kajala Akwaa Skendo Kisa Penzi la Harmonize… Mwijaku na H.Baba ‘Wasepeshwa’

0
Kakaja Masanja.

KAJALA Masanja anakula tamu na chungu ya penzi la msanii  Rajab Abdul Kahar ‘Harmonize’. Pengine ndiyo maana  Waswahili walisema, huwezi kula muwa bila kuvuka fundo.

Inawezekana kwa hali ilivyo Kajala sasa anavuma kwa skendo ya Kiswahili inayomtafsiri kama mwanamke mwenye changamoto kwenye mapenzi.

 

Panda shuka ya penzi la mastaa hao sasa linaonekana kumtwika mzigo Kajala, maana mjadala uliopo kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu kuporomoka kwa Lebo ya Konde Gang inayomilikiwa na Harmonize.

Kwa imani za Kiswahili mwanaume akioa na mambo yake ya maisha kuanza kumwendea kombo mtuhumiwa wa kwanza atakuwa mke.

 

Wakwe, mawifi na mashemeji wataanza kumuona ndugu yao kama kaoa mwanamke ambaye hawaendani naye nyota.

Andiko kwenye mtandao wa kijamii kutoka kwa mtu mmoja linasema tangu penzi la Kajala na Harmo lianze Lebo ya Konde ilianza kuporomoka.

 

Chawa wa lebo, meneja, wasanii chipukizi, walinzi na wapambe wengi wameshika hamsini zao.

Mwijaku na H.Baba walikuwa chawa wazuri wa Harmonize lakini sasa hivi wamehamia ‘kambi ya upinzani’ kumshambulia msanii huyo.

Harmonize akiwa na mpenzi wake Kajala.

Mjerumani ambaye ni meneja mzoefu naye alijitoa kwenye Lebo na sasa kuna wasanii chipukizi kama Cheed na Killy wametemwa kwenye lebo.

 

Tatizo nini? Ndiyo hapo unapokuja mjadala unaomhusu Kajala kwamba; huenda amepeleka nguvu ya tofauti kwa Harmonize.

Wapo wanaosema amekuwa na sauti kubwa ndani ya lebo huku wengine wakidai asali ya penzi aliyopa Harmo imemlevya msanii huyo kiasi cha kuwasahau wengine.

 

Kama yote hayo yanaweza kuwa maganda basi chungwa linawezekana kupatikana kwa hoja ya matumizi makubwa ya fedha ambayo yanaifanya lebo ishindwe kujiendesha.

 

Maana inadaiwa kuwa Kajala huwa haangukii kwenye mikono mitupu na mwenyewe mara kadhaa amekuwa akitamba kuwa akimpata mwanaume saizi yake “hachomoki.”

 

Wengine wanakumbushia maisha ya Kajala na mumewe wa kwanza Faraji Agustino yalivyokuwa ya anasa lakini walijikuta kifungoni kwa tuhuma za ufisadi.

 

Hawa ndiyo Waswahili; lakini ukweli wa kitaalam, msanii kumiliki lebo katika wakati ambao uchumi wa dunia umetikisika siyo kazi rahisi.

Huenda hii ikawa sababu  kuu yenye maana iliyomfanya Harmo aachane na wasanii hao. Je, wasanii hao chipukizi hawakuwa wabunifu na watu wa kujituma?.

 

Yamesemwa na yataendelea kusemwa, lakini kwa ahadi Ijumaa litamtafuta bosi wa Konde Gang Harmonize a.k.a Tembo lipige naye stori mbili tatu.

Stori: Na Richard Manyota, Ijumaa

MASHABIKI SIMBA HAWAJARIDHISHWA na MATOKEO WATAKA USAJILI MWINGINE DIRISHA DOGO..

Leave A Reply