Kaka Ashirikiana na Mama Kumchinja Dada Yake

POLISI katika Jimbo la Maharashtra katika Wilaya ya Aurangabad, Mumbai nchini India wamewakamata kijana mmoja na mama yake kwa madai ya kumkata kichwa dada yake aliyekuwa mjamzito, tukio ambalo amelitekeleza Jumapili iliyopita, Desemba 5, 2021.

 

Polisi wamesema binti huyo aliyefahamika kwa jina la Kirti Thore (19) aliolewa kisiri na mwanamume bila idhini ya familia yake tangu mwezi Juni mwaka huu, hali iliyoibua chuki baina yao.

 

Imeelezwa kuwa, kabla ya kutekeleza mauaji hayo, mama alimpigia simu binti yake na kumweleza kuwa wangependa kumtembelea nyumbani kwake anapoishi na mumewe, binti huyo aliwakaribisha na kuwaelekeza nyumbani kwake.

Ilipofika Jumapili, mama na kijana wake walifunga safari kwenda anakoishi binti huyo ambapo mara baada ya kufika, walimkuta binti huku mumewe akiwa chumba kingine, bila kupoteza muda, kaka mtu alimkaba shingo dada yake huyo aliyekuwa mjamzito na kumchinja kwa mundu huku mama mtu akiwa ameshikilia miguu.

 

Baada ya hapo kijana alianza kumsaka shemeji yake ndani ya nyumba hiyo ambaye alikimbilia jikoni na kufanikiwa kutoroka.

 

Kijana huyo alikizungusha kichwa cha dada yake hewani mara kadhaa na kujipiga selfie kabla ya kukitoa nje ili majirani waone na kukitupa kwenye veranda, kabla ya kujisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Virgoan, maofisa wa usalama wamesema.


Toa comment