The House of Favourite Newspapers

Kaka wa Kim Jong-un Aliyeuawa, Alikuwa Jasusi wa CIA

IMERIPOTIWA kwamba kaka wa kambo wa Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un,  aliyeitwa Kim Jong-nam aliuawa kwa sumu akiwa safarini nchini Malaysia mwaka 2017, baada ya kubainika kuwa ni jasusi wa shirika  la ujasusi la Marekani CIA.

 

Gazeti la Wall Street Journal, limechapisha ripoti hiyo Jumatatu na kusema limedokezwa hayo na mtu mwenye taarifa kamili kuhusu tukio hilo na kwamba kulikuwa na mawasiliano baina ya CIA na Kim Jong-nam.

Uchunguzi uliofanywa na Malaysia kuhusu kesi hiyo mwaka jana uligundua kuwa, Kim Jong-nam alikutana na raia mmoja wa Marekani, aliyeshukiwa kuwa ni jasusi, katika hoteli moja nchini Malaysia siku nne kabla ya kuuawa tarehe 9 Februari 2019.

 

Kabla ya hapo, raia mmoja wa Indonesia, Siti Aisyah, na raia mmoja wa Vietnam, Doan Thi Huong, walikuwa wamekamatwa kwa tuhuma za kumpa sumu Kim Jong-nam katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, lakini waliachiliwa huru mapema mwaka huu nchini Malaysia baada ya kukosekana ushahidi.

Marekani na Korea Kaskazini zina historia ndefu ya uhasama na uadui. Mwaka jana Rais Donald Trump wa Marekani alikutana na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, nchini Singapore kwa ajili ya mazungumzo ya kuthibiti silaha za nyuklia.

 

Walifanya mkutano wa pili mjini Hanoi, Vietnam, mapema mwaka huu lakini mazungumzo hayo yaligonga mwamba baada ya Korea Kaskazini kuituhumu Washington kuwa imepoteza fursa nadra ya kupunguza uhasama.

 

WATU 10 MATAJIRI ZAIDI KUWAHI KUTOKEA DUNIANI!

Comments are closed.