Taifa Stars Kuanza kazi kwa kukipiga dhidi ya Misri kesho

WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wakiwa kwenye mazoezi yanayofanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Olympics Center Maadi jijini Cairo, timu hiyo imeweka kambi nchini Misri kujiandaa na mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019).

 

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Juni 21, mwaka huu lakini keshokutwa Ijumaa jioni, Taifa Stars itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji hao, Misri ikiwa ni sehemu ya kujiandaa kwa michuano hiyo.

 

Wakati Taifa Stars ikiendelea na mazoezi, juzi ilitembelewa na Watanzania waishio nchini

Misri ambapo walihojiwa na kusema kuwa wapo tayari kuisapoti timu yao ya taifa na watashangilia katika michezo yote ambayo itacheza ndani ya michuano hiyo.

 

Akizungumza kwa niaba ya wenzake kadhaa waliofika uwanjani hapo, Abdul Salala alisema: “Mimi ni Mtanzania, nipo hapa Misri kwa ajili ya masomo, mimi na wenzangu tuko tayari kuiunga mkono timu yetu, sisi ni wazalendo, niwaambie Watanzania waliopo nyumbani, wasiwe na wasiwasi, tunaiamini timu yetu itapata ushindi kutokana na kuonekana kuwa na maandalizi mazuri.”

 

Akizungumzia kambi hiyo, Meneja wa Taifa Start, Daniel Msangi alisema:

“Vijana wanaendelea vizuri na kambi, kesho (leo) tunatarajiwa kusafiri kuelekea Alexandria kwa ajili ya kucheza mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya Misri, kocha Emmanuel Ammunike anaendelea vizuri na kambi.

“Ukweli ni kuwa kambi yetu iko vizuri na kuna vifaa vyote muhimu.”


Loading...

Toa comment