Kamati ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge imependekeza Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Conchesta Rwamlaza asimamishwe kuhudhuria vikao vitatu vya mkutano wa saba unaoendelea wa Bunge la bajeti baada ya kumtia hatiani kwa kusema uongo.
Julai 11 mwaka jana akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rwamlaza alimtuhumu Mbunge wa Muleba Kusini (CCM) Profesa Anne Tibaijuka kuwa wakati akiwa Waziri wa wizara hiyo alitumia vibaya madaraka yake.
Rwamlaza alimtuhumu Tibaijuka kwa kujimilikisha zaidi ya ekari 4000 katika Kijiji cha Kyamnyorwa na kwamba kiasi hicho cha ardhi ni zaidi ya kiasi alichoomba kihalali ambacho ni ekari 1098.
Akisoma mapendekezo ya kamati hiyo leo (Jumatano) mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika amesema kauli hizo zilimshushia heshima Profesa Tibaijuka mbele ya Bunge na jamii anayoiongoza.
Pia amesema kauli hiyo zilikuwa zikimgombanisha Profesa Tibaijuka na wananchi wa eneo hilo ambalo lipo ndani ya jimbo lake.
Bunge la Tanzania limetenga chumba maalumu kwa ajili ya wabunge wanawake kuwanyonyeshea watoto wao wakati vikao vya Bunge vikiendelea. pic.twitter.com/8K4Cs5vq1F
— Global Publishers (@GlobalHabari) June 28, 2017
Wabunge kwa pamoja waafiki kumsamehe Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari aliyekuwa akituhumiwa kuvuruga shughuli za bunge kwa kelele. pic.twitter.com/YIPkROViYC
— Global Publishers (@GlobalHabari) June 28, 2017
Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imemuachia huru MwenyeKiti wa CHADEMA Lindi, Suleiman Mathew na Katibu wa Tawi la Nyangamara, I. Kupilil. pic.twitter.com/MIGFGZgBhS
— Global Publishers (@GlobalHabari) June 28, 2017