The House of Favourite Newspapers

Kampuni ya Kansai Plascon Yazindua Rangi Mpya

0
Kutoka Kushoto;  Mkuu was Mauzo Kansai Paint Tanzania Jamal Hussein, Solomon NIcholas ,  Mkurugenzi Mtendaji Kansai Plascon Tanzania,  Lucas Mhuville (Joti) – Balozi wa Plascon Tanzania Olympia Fraten,  Mkuu wa Masoko Kansai Plascon FLora Mapunda  na Mkuu wa Mauzo Kansai Paint Dar es Salaam

Dar es Salaam Jumanne 11 Mei 2021: Kampuni ya Kansai Plascon imezindua rangi mpya na kubadili muonekano wa nembo za bidhaa zake pendwa, zenye ubora wa hali ya Juu katika kampeni yao inayojulikana kama Plascon ni zaidi ya Rangi.

Soko la rangi nchini Tanzania limekuwa likiongezeka kutokana na ukuaji mkubwa wa idadi ya watu wanaoishi mjini, kuongezeka kwa watu wenye maisha ya kati, sera za serikali zinazounga mkono maendeleo ya miundombinu na kuongezeka kwa uhamiaji mijini. Rangi za mapambo ni sehemu kubwa ya biashara ya rangi nchini.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi mtendaji wa Kansai Plascon, Bw. Hussein Jamal leo Mei 11, 2021 alisema “Soko la rangi nchini Tanzania lina ushindani mkubwa. Kampuni ya Kansai Plascon inaongoza kwa ubora na uvumbuzi wa bidhaa za kisasa Zaidi kupitia taasisi zake za utafiti zilizopo Japani, India na Afrika Kusini.

 

Pia Plascon imewekeza katika miundombinu nchini Tanzania inayoongeza uwezo wa kutengeneza rangi za aina mbalimbali. Pia Plascon imewekeza katika miundombinu nchini Tanzania inayoongeza uwezo wetu wa kutengeneza rangi za aina nyingi na kutufanya tuwe vinara wa rangi bora za mapambo na magari nchini.”

Aliongeza kuwa “Kupitia utafiti na uvumbuzi, Kansai Plascon imetambulisha muonekano mpya wa rangi zake zenye ubora wa hali ya juu za; Plascon Weatherguard, Plascon Vinyl Silk na Plascon Super Gloss. Pia Plascon imetambulisha kwa mara ya kwanza rangi yake mpya ya Plascon Anti Mosquito Paint,”

 

Rangi za Plascon zina ubora wa hali ya juu na zina faida zaidi ya rangi ya kawaida; 1) Plascon Anti Mosquito Paint ni rangi mpya kabisa na ni ya kwanza Tanzania yenye uwezo wa kuua mbu muda mfupi baada ya kutua ukutani

2) Rangi ya Plascon Weatherguard ni rangi namba moja ya kuzuia ukungu na fangasi kwenye jengo na inahimili mabadiliko ya hali ya hewa

3) Rangi ya Plascon Vinyl Silk inadumu muda mrefu, rahisi kusafisha kuta zako na haipauki.

4) Rangi ya Plascon Super Gloss inauwezo mkubwa wa kulinda na kufunika sehemu mbali mbali zikiwemo kuta za jengo, mbao na chuma.

Kansai Plascon wana rangi zaidi ya 5000 na zinapatikana madukani kote nchini na kwa kupitia mawakala wetu.

Kampuni ya Kansai Plascon katika kampeni yake ya PLASCON NI ZAIDI YA RANGI, imemtambulisha rasmi Msanii Lucas Mhuvile almaarufu kama Joti na Nishai kuwa balozi wa rangi za Plascon na kuwa fundi rangi namba moja Tanzania.

 

Kwa upande wake Nishai alisema “Ninayo furaha kubwa sana kujiunga na familia ya Plascon na kupata mafunzo ya upakaji rangi. Nitatembea nchi nzima nikitoa mafunzo na kuongea na mafundi wenzangu na wateja ili kuwadhirishia ubora wa rangi za Plascon na kuonyesha jinsi Plascon ni Zaidi ya rangi za kawaida.”

 

Aliongeza “Wananchi wote wanauwezo wa kupata taarifa mbalimbali kuhusu rangi za Plascon na kuzungumza moja kwa moja na mimi kupitia mitandao yangu ya kijamii, na nitazidi kutoa mafunzo na ushauri kupitia Whatsapp namba 0737 72 71 83 ili kuongeza uelewa wa utaalamu huu wa kupaka rangi kwa wananchi.”

 

Kuhusu Kampuni ya Kansai Paint 

Makao makuu ya Kansai Paint yapo nchini Japan, na ipo kwenye orodha ya makampuni 10 makubwa zaidi ya rangi dunian na ni moja ya kampuni za rangi zinazo ongoza duniani kwa ubora wa rangi za magari na majengo. Kansai Paint ni kampuni inayoongoza kwa Ubora na Utoaji wa bidhaa zinazo kidhi mahitaji ya wananchi kwenye soko la Afrika Mashiriki.

Mawasiliano: 

0713900698 or 022 2865141/2

www.kansaiplascon.co.tz

https://www.facebook.com/PlasconTZ

https://www.instagram.com/plascontanzania/

 

Leave A Reply