The House of Favourite Newspapers

Mkuu wa Wilaya Kibiti Afungua Mafunzo ya Kamati ya Ulinzi

0

Mkuu wa Wilaya Kibiti, Gulam Hussein Kifu, Mei 11, 2021 amefungua mafunzo ya kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto katika ngazi ya kata,ambapo mafunzo hayo yalifanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya huyo, na mafunzo hayo yamewezeshwa kwa ufadhili wa NCA (Norwagian Church Aid)

Katika mafunzo hayo,Mkuu wa wilaya huyo alizungumzia,kuzingatia kupinga ukatili wa kijinsia unaofanywa wilayani humo na familia nyingi,zinaficha maovu yanaofanyika kwa kuogopana kuvunja undugu,maana wengine wanaishi na ndugu zao na wanawafanyia ukatili watoto zao na kunyamaza kimya.

Na kwa upande wa mwezeshaji wa semina hiyo,kutoka NCA, Agatha Lema, alisema kuwa anashukuru sana angalau kwa sasa wakazi wa Kibiti,wameanza kuwa na uelewa mkubwa sana ,kuhusiana na kufichua maovu ya ukatili wa kijamii kwenys familia.

 

Leave A Reply