The House of Favourite Newspapers

KAMPUNI YA KIGANJANI KUKOPESHA HUDUMA ZA LUKU WATEJA WAKE

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kiganjani Sercices Ltd, Fredy Felician, (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Mkurugenzi wa Oparesheni wa Kampuni ya Kiganjani Sercices Ltd, Qs. Mhonda Joseph (kushoto) akitoa ufafanuzi.

 

 

KAMUNI ya Kiganjani Sercices Ltd imekuja na huduma yake mpya ijulikanayo kama ‘Kopa Umeme Kiganjani Mwako’ ambayo imetambulishwa leo kuwa hivi karibuni itazinduliwa rasmi ikitoa huduma za kukopesha huduma za luku kupitia simu za mkononi.

 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Fredy Felician, ameeleza kuwa watanzania wakae mkao wa kula kuipokea huduma hiyo mpya ambayo itakuwa ikitolewa  kupitia simu za mkononi na jitihada zinaendelea za kukamilisha taratibu.

 

 

Ameeleza kuwa makampuni kama vile Vodacom,Tigo, TTCL na bank kama vile CRDB zimeridhia  kuwezesha upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa jamii.

 

 

“Tunafurahi sisi kama kampuni ya kizalendo  naya kipekee kubuni wazo hili ambapo COSOTA wametupa cheti cha hatimiliki, hivyo watanzania watanufaika na  huduma hii ambayo itakuwa mwokozi kwao maana hakuna ambaye atalala giza au kukwama kwenye shughuli za kiuchumi eti sababu hana pesa,”alisema Felician.

 

 

Aidha ameeleza kwamba Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  na Wizara ya Nishati zimewapa ruhusa kuendelea na taratibu za utoaji wa huduma hiyo ambayo kazi yake itakuwa ni kuwakopesha wateja wao kiasi cha fedha kupitia manunuzi ya umeme kwa njia ya simu za mkononi na baadaye wateja wao kurudisha kulingana na maelekezo yatakavyo waelekeza na muda husika.

Comments are closed.