The House of Favourite Newspapers

MV NYERERE: PICHA 9 KUTOKA ENEO LA TUKIO, HALI ILIVYO

MAJONZI MAZITO! Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwelwe amesema uokoaji wa miili ya waliofariki dunia baada ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere utakamilika leo Septemba 21, 2018 kabla ya saa 12 jioni huku lengo likiwa ni kuhakikisha wanawaokoa wote walionasa kwenye kivuko hicho.

Kamwelwe ametoa kauli hiyo leo mchana wakati akihojiwa na kituo cha Utangazaji cha Taifa (TBC), akiwa eneo la tukio Kisiwa cha Ukara wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.

Mpaka sasa miili zaidi ya 100 imepatikana katika ajali hiyo kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.

Kwa mujibu wa mashuhuda, kivuko hicho kilikuwa na zaidi ya abiria 400 ambapo majeruhi takribani 40 ambao wameokolewa na kupelekwa Kituo cha Afya Bwasha, Ukara kupatiwa matibabu na wengine wengi wakihofiwa kufa maji.

PICHA NA IDD MUMBA | GLOBAL PUBLISHERS, UKEREWE

MV NYERERE: Tazama Miili ya Watu Ikiopolewa Ziwa Victoria, Inahuzunisha!

Comments are closed.