The House of Favourite Newspapers

Kamusoko, Ngoma waleta fowadi

0

Nicodemus Jonas,
Dar es Salaam
UWEZO unaoonyeshwa na wachezaji wawili wa Yanga, raia wa Zimbabwe, straika Donald Ngoma na kiungo Thaban Kamusoko, umemfanya kocha wa Mbeya City, Kinnah Phiri, atangaze kuwa ataongeza straika mmoja kutoka kwenye nchi hiyo.
Akifafanua kwa ukina wake, kocha huyo wa zamani wa Free States ya Afrika Kusini, alisema Zimbabwe ni miongoni mwa nchi zenye wachezaji wengi wenye viwango vya juu kwenye soka la Tanzania, akiwatolea mfano Ngoma na Kamusoko walivyotegemeo la Yanga kwa kila kitu.

“Nawajua vizuri Wazimbabwe, ni moja ya nchi zenye wachezaji wazuri, mfano mzuri angalia Ngoma na yule mwenzake wanavyofanya vizuri pale Yanga. Pia timu kama Chicken Inn kuna wachezaji wengi wazuri ambao wanaweza kukusaidia.

“Kikubwa lazima tuboreshe safu ya ushambuliaji na ningeomba sana kama ningepata wa kimataifa lakini iwapo viongozi watakataa, hakutakuwa na jinsi nitasajili humuhumu ingawa kipaumbele zaidi ingekuwa kimataifa,” alisema.
Katika mikakati yake, amepanga kupata mmoja wa kimataifa na wengine wawili wa kitaifa katika nafasi nyingine.

Leave A Reply