The House of Favourite Newspapers

Kanda Ya Kati Waitaka Nyumba Mpya Ya Pili Ya Global

13529116_1206494709383398_8104726601975312744_nNyumba ya Global aliyojishindia Nelly Mwangosi.

GLOBAL Publishers, kampuni namba moja ya uchapishaji wa magazeti Tanzania, imetangaza nia yake ya kutoa nyumba ili ishindaniwe na wasomaji wa magazeti yake, ambayo ni Championi, Risasi, Ijumaa, Uwazi na Amani.

DROO NDOGO YA SHINDA NYUMBA (2)Shinda nyumba ya kwanza: Msomaji akizidi kuchanganya kuponi hizo.

Hii itakuwa ni mara ya pili ndani ya mwaka mmoja, kwa Global Publishers kutoa nyumba kwa ajili ya wasomaji wake, kwani miezi sita iliyopita, katika bahati nasibu iliyofahamika kama Shinda Nyumba, Nelly Mwangosi, mama wa watoto wawili mkazi wa Iringa, alijishindia mjengo wenye thamani ya mamilioni ya shilingi, ambao ulikuwa na kila kitu ndani, uliojengwa huko Salasala, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

DROO NDOGO YA SHINDA NYUMBA (8) DROO NDOGO YA SHINDA NYUMBA (9)Shinda nyumba ya kwanza: Msimamizi Mwandamizi Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Chiku Saleh (wa kwanza kushoto) akishuhudia jina la mmoja wa washindi waliopatikana baada ya droo.

Siku chache tu baada ya Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho kutangaza nia hiyo, mamia ya wasomaji kutoka kila pembe ya nchi wamekuwa wakipiga simu katika chumba cha habari na kutaka taarifa kamili juu ya siku hasa ya kuanza kwa promosheni hiyo, kwani kukosa kwao nyumba katika awamu ya kwanza, kuliwapa hamasa ya kutaka kujaribu tena.
Chumba cha habari cha gazeti hili kiliwasiliana na wasomaji wengi kutoka Kanda ya Kati, ambao walisema kama ni kikanda, basi zamu hii ni yao kwa vile mshindi wa shindano lililopita, alitokea Nyanda za Juu Kusini.
Akizungumza kwa njia ya simu kutokea Hombolo, mkoani Dodoma, Gido Chipondi alisema amekuwa msomaji mzuri wa magazeti ya Global Publishers kwa miaka mingi na kushiriki promosheni zote huku akishinda zawadi ndogondogo, lakini anaamini safari hii, zawadi kubwa kabisa itatua kama siyo mkoani Dodoma, basi ni kanda ya kati.
“Kuhusu kuamini mimi sina tatizo hata kidogo na Global, ninajua wakiamua kutangaza kitu huwa wanafanya, lakini sikumbuki kama kuna mshindi wa zawadi kubwa zinazotangazwa aliwahi kutoka Dodoma au Kanda ya Kati, nadhani hii ni zamu yetu, binafsi hakuna gazeti nitakalolikosa,” alisema.
Msomaji mwingine aliyepiga simu kutokea Bahi, mkoani Dodoma, Samson Mbopoma alisema watu wengi wameamini kuwa hakukuwa na upendeleo katika bahati nasibu hiyo ya kwanza baada ya kuona mshindi hakuwa mtu wa Dar es Salaam.
“Tunajuaga bahati nasibu nyingi zinakuwaga usanii tu, wanajipanga wenyewe ili kushinda, lakini baada ya mshindi kuwa ni mwenyeji wa Iringa, binafsi nilijenga imani kubwa sana na Global, nionavyo safari hii Dodoma itaibuka kinara kwenye hiyo nyumba,” alisema Mbopoma.
Rehema Mpumpa wa Ikungi, aliyepiga simu akiwa haamini kama shindano hilo linarudi tena, alisema kwa jinsi alivyopania, anaamini Mungu atamlipa kwani kwa miaka mingi, amekuwa ni mteja mzuri wa magazeti ya Global Publishers.
“Mimi kwa kweli nimuombe tu Mungu anisaidie niibuke mshindi, lakini kama nitakosa, basi apate mtu wa Singida na ikishindikana kabisa, awe kutoka Kanda ya Kati, maana wenzetu kule Iringa wameshapata mwakilishi wao,” alisema Rehema.
Wasomaji wengine waliopiga simu chumba cha habari ni Juma Nkhanga wa Kititimo Singida, Ramadhani Juma wa Ilongelo, Singida vijijini na Miriam Ntunde wa Singida mjini.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, alisema jana kuwa wakati wowote mwezi huu watatangaza siku rasmi ya kuanza kwa mchakato wa tukio hilo kubwa.
Katika droo ya Shinda Nyumba iliyochezeshwa mapema mwaka huu, licha ya zawadi ya nyumba ya kisasa iliyokuwa na samani zake ndani, zawadi zingine ndogondogo zilitolewa, zikiwemo pikipiki, flat screen tv, mashuka, mablanketi, vyombo vya jikoni, fulana, kofia na vitu vingine vingi, vyote kwa pamoja vikigharimu mamilioni ya fedha.

WASANII WA BONGO MUVI NA BONGO FLEVA WALIVYOTEMBELEA JUMBA LA MSHINDI WA SHINDA NYUMBA

Comments are closed.