The House of Favourite Newspapers

Lugola: Magufuli ni Kama Yesu – Video

0

Bunge la 11 limeendelea bungeni jijini Dodoma ambapo leo Juni 13, 2020 mjadala wa bajeti kuu umeendelea huku wabunge mbalimbali wakipewa fursa ya kuchangia bajeti hiyo.

 

Na hizi ndizo kauli za Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola akichangia bungeni leo; “Tunapokuwa na Rais wa namna hii [kama Rais Magufuli] hatuhitaji tena kuingia kwenye mjadala wala michakato ya kutafuta Rais mwingine, kwa sababu huyu Rais wa Watanzania tayari amekwisha patikana.

 

“Rais Magufuli amekuwa kama Yesu Kristo, Watanzania wanamlilia na kumfuata na ndiyo maana hata aliponitengua nilisema, ulinipa heshima ya huu Uwaziri na leo umeutwaa, jina la Magufuli libarikiwe.

 

“Niliwahi kusema watu kama Rais Magufuli hawazaliwi kila wakati na hauwezi kuwapata kila mahala, watu ambao unaweza kuwapata kila mahala ni walevi kama kina
Freeman Mbowe na Rais Magufuli ninamfananisha kama Mwenge wa Uhuru.

 

Leave A Reply