The House of Favourite Newspapers

Kanisa la Victory Christian Centre Lazindua Tamasha la ‘Campus Night’

0

KANISA la Victory Christian Centre (VCCT) chini ya Mchungaji Kiongozi Dk. Huruma Nkone leo limezindua maandalizi ya kongamano la kihistoria kwa mwaka 2016 lijulikanalo kwa jina la “CAMPUS NIGHT” .
Uzinduzi huo unalenga kuwaweka pamoja wanafunzi wenye imani na dini mbalimbali kutoka vyuo mbalimbali katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo tamasha hilo limekuwa likikua kwa kasi kubwa tangu kuasisiwa kwake mwaka 2005 na idadi ya wanafunzi wanaohudhuria inaonesha kupanda kutoka 2,500 mwaka 2005 hadi 12,000 mwaka 2009 na 15,000 mwaka 2011.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Dk. Nkone alisema kuwa tukio la Campus Night hutanguliwa na mipango mbalimbali ambayo hufanyika siku kadhaa kabla ya tukio lenyewe ambapo mambo kama vile bonanza la michezo, maonesho ya kitaaluma, ushauri na upimaji yatafanyika.
Aliongeza kwamba mipango hiyo huhitimishwa na mada za uimbaji wa wanafunzi na uchekeshaji.
Aidha Dk. Nkone alisema kuwa lengo la Campus Night ni kuwafikia wanafunzi ili waweze kuimarisha maisha yao ya kiroho, kimaadili, kiuongozi na pia hutoa fursa kwa wanafunzi kujifunza masuala muhimu kwa ajili ya maisha yao ya sasa na baadaye.
Alifafanua kuwa kwa kupitia Campus Night maisha ya vijana wengi yamefanikiwa kubadilika sana kiroho na kimaadili.
“Tumeandaa wananchi wema na wazalendo, viongozi mahiri wenye mtazamo wa kimaendeleo na mafanikio. Wanafunzi wanaoanza mwaka wa kwanza wanafaidika kwa kupata ufahamu wa maisha ya chuo kupitia uzoefu wa shuhuda za watu waliofanikiwa na hata wanaohitimu huweza kupambana na changamoto za wanakokwenda.
Aliitaja siku ya Kongamano hilo kuwa ni Novemba 11 mwaka huu ambapo litafanyika katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar es Salaam l na litaanza muda wa saa 12:00 jioni hadi saa 11 alfajiri.
Mchungaji huyo anawakaribisha wanafunzi wote katika kongamano hilo la kihistoria la 2016 lenye kauli mbiu isemayo ”Badilika toka ndani kwenda nje” na miongoni mwa wazungumzaji katika kongamano hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, Dk. Chris Mauki, Mkurugenzi wa Victory Campus Night Prosper Mwakitalima, na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba.

campas-night-vcc-1

Mchungaji Kiongozi Dk. Huruma Nkone akizungumza jambo katika uzinduzi huo.

campas-night-vcc-2

…Akisisitiza jambo katika uzinduzi huo.

campas-night-vcc-3

Baadhi ya waumini wa Kanisa la Victory Christian Centre wakifuatilia uzinduzi huo kanisani hapo.

campas-night-vcc-4

Mabango yanayoonesha kukamilika kwa uzinduzi huo yaliyoandikwa “Campus Night”.

campas-night-vcc-6

Dk. Chris akihojiwa na wanahabari.

campas-night-vcc-7

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wakiendelea na ibaada baada ya kukamilika kwa shughuli ya uzinduzi.

eric-shigongo

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, akihojiwa na wanahabari baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo namna alivyojipanga kwa ajili ya kongamano hilo.

upendo-nkone

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Upendo Nkone, akihojiwa na wanahabari kuhusu tukio hilo.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply