The House of Favourite Newspapers

Efm Wasepa na Kijiji, Temeke Dar

0

 

KITUO cha Redio cha Efmkilichopo Kawe-Mikocheni jijini Dar, chini ya Udhamini wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom usiku wa kuamkia leo Jumapili ilitua Wilaya ya Temeke katika Baa ya New Bulyaga na kusepa na kijiji katika tamasha lao lijulikano kama Muziki Mnene.
Katika tamasha hilo, burudani ilikuwa ya aina yake na shangwe kila kona kutoka kwa mashabiki waliofurika katika baa hiyo pale walipokuwa wakipanda wasanii wanaokuja kwa kasi kupitia Muziki wa Singeli.
Tamasha hilo, lilizinduliwa rasmi Agosti 27, mwaka huu ambapo,Meneja wa Efm, Dennis Ssebo alisema lengo kubwa ni kukutana na kuwashukuru wasikilizaji wao katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar na Mkoa wa Pwani, kwa namna walivyoipokea Efm Radio na kushirikiana nao hadi kufikia sasa.
Alisema tamasha la muziki mnene mwaka huu linafanyika kwa kipindi cha muda wa miezi mitatu ambapo muziki unapigwa katika baa 12 za jiji la Dar na Pwani likiwa limebeba kauli mbiu ya ”TUNASEPA NA KIJIJI” ikiwa na maana kuwa, kila wiki Efm inaweka kambi katika kijiji kimoja ama eneo moja kwa muda wa siku nne.
Aidha muziki mnene eneo husika unapokuwa umetua huenda sanjari na kampeni ijulikanayo ‘NJE NDANI’ ambapo vipindi vinne vinarushwa moja kwa moja (live) katika mtaa husika ambavyo ni Uhondo (Siku ya Jumatano), Sports Headquarters (Alhamisi), Joto la Asubuhi (Ijumaa) pamoja na Funga Mtaa (Jumamosi) na burudani kutoka kwa RDJ’s Mamy wa Efm.
Pia kwa muda wa asubuhi,Muziki Mnene unapokuwa umetua panakuwa na Jogging, Muziki waSingeli, michano kutafuta vipaji vya wasanii wa muziki ambapo anayeibuka mshindi hupewa fursa ya kupigiwa nyimbo zake kupitia radio hiyo na mpira wa miguu kati ya Timu ya Efm na Timu za Maveterans wa eneo husika.

1-mashabiki-wa-redio-efm-93-7-waliojitokeza-katika-baa-ya-new-buylaga-wakishuhudia-burudani-hiyo

Mashabiki wa Redio Efm, 93.7 waliojitokeza katika baa ya New Buylaga wakishuhudia burudani hiyo.

2

RDJ’s Mamy wa Efm 93.7 akifanya yake.

3-mmoja-wa-wanamuziki-chipukizi-wa-nyimbo-za-singeli-akitoa-burudani

Mmoja wa wanamuziki chipukizi wa Singeli akitoa burudani.

4-mwanamuziki-chipukizi-wa-singeli-akiwaburudisha-wasikilizaji-wa-redio-efm

Mwanamuziki wa Singeli akiendelea kuwaburudisha wasikilizaji wa redio Efm.

5-burudani-mwanzo-mwisho

Burudani mwanzo mwisho.

6-burudani-ikiendelea

Shangwe za burudani zikiendele katika baa hiyo.
NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply