The House of Favourite Newspapers

KARRUECHE KAMA UKO SINGLE WIVU WA NINI KWA QUAVO NA NICK MINAJ?

0

WAHENGA walinena mapenzi ni kikohozi kuyaficha huwezi na msemo huu unajidhihirisha kwa mwanamitindo ambaye pia ni muigizaji kutoka pande za Marekani, Karrueche Tran, ambaye anaugulia kidonda cha wivu wa mapenzi licha ya kuweka wazi kwamba tangu aachane na mpenzi wake , Chris Brown, hana mpenzi yaani yupo ‘single’.

 

Hivi karibuni alionekana akiwa karibu sana na msanii ambaye anaunda kundi la ‘Rap Group Migos’, Quavo, kiasi cha kufanya watu kuhisi huenda wawili hawa wapo kwenye dimbwi la mahaba, lakini Karrueche alipoulizwa aling’aka na kusema kwamba yupo single.

 

Ugonjwa wa wivu ulianza kumtesa baada ya Quavo kuhamisha majeshi na kuwa karibu na rapa nguli nchini Marekani, Nick Minaj, ambapo ukaribu huo unasababishwa na harakati za kushuti video ya wimbo wao.
Karrueche ameonekana akiwa mpweke baada ya kuwa mbali na Quavo kwa muda kidogo, hali iliyowafanya mashabiki kusema anaona wivu.

NA ISRI MOHAMED/GPL

Leave A Reply