The House of Favourite Newspapers

Karrueche Tran amwaga machozi Nigeria kituo cha yatima

0

imageMwanamitindo maarufu duniani, Karrueche Tran akiwa na watoto yatima hao.

MWANAMITINDO maarufu duniani, Karrueche Tran, hivi karibuni alimwaga machozi kutokana na kushindwa kuzizuia hisia zake alipokutana na watoto yatima wanaotunzwa katika Kituo cha Internally Displaced Persons (IDP) huko Abuja, Nigeria.

Baada ya tukio hilo mwanamitindo huyo mabaye kwa sasa yupo nchini Nigeria kwa ajili ya kutembelea kituo hicho na kuongea na watoto yatima katika hali ya kuwatia moyo, aliposti picha nyingi kwenye ukurasa wake wa Instagram zikimuonyesha akiwa  na watoto hao huku akielezea jinsi alivyowaonea huruma kutokana na maisha wanayoishi.

image (1)“Nikiwa kwenye kambi ya IDP nilipata bahati ya kuzungumza na watoto juu ya maisha yao pamoja na historia zao, kiukweli zilikuwa zinaumiza kiasi kwamba nilishindwa kuvumilia na kumwaga machozi,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Leave A Reply