The House of Favourite Newspapers

Kaseja: Nipo tayari Kuwavaa Kenya Jumapili

Juma Kaseja

MLINDA mlango mkongwe nchini, Juma Kaseja ametamba kuwazuia washambuliaji wa timu ya taifa ya Kenya kwenye mechi ya kufuzu michuano ya CHAN itakayopigwa Jumapili Julai 28, Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Kaseja ambaye mara ya mwisho kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ilikuwa mwaka 2013, amesema kuwa anaamini kuwa anaweza kufanya mambo makubwa. Kaseja ameliambia Championi Jumatano kuwa jambo kubwa kwa mchezaji ni kuwaza jinsi gani ya kulisaidia taifa lake.

 

“Kwa sasa nina majukumu na timu ya taifa na jukumu lenyewe ni kuhakikisha nalisaidia taifa langu katika mchezo dhidi ya Kenya, hilo siku zote ni jukumu la kila mchezaji kuhakiki-kisha analisaidia taifa lake.

 

“Naamini kuwa tutafanya vizuri kwenye mchezo wetu kwa kuwa wote tupo kwenye morali ya juu,” alisema kipa huyo.

Comments are closed.