The House of Favourite Newspapers

Kaseke: Subiri Muone Singida Utd ni Timu Bora

0
Deus Kaseke.

 

KIUNGO wa zamani wa Klabu ya Yanga, Deus Kaseke amesema japokuwa wamepoteza mechi yao ya kirafiki dhidi ya timu yake hiyo ya zamani, kwake Singida United ni bora yenye kiwango kikubwa.

 

Kaseke, kiungo wa zamani wa Mbeya City na Yanga, juzi aliitumikia timu yake mpya hiyo na kupoteza kwa kufungwa mabao 3-2 mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Akizungumza na Championi Jumtatu, Kaseke alisema kuwa anafuraha ya kujiunga tena na kocha wake wa zamani na kusema kuwa atafanya juhudi zake kuisaidia timu yake mpya msimu ujao kwani kupoteza mechi yao ya kirafiki haijaharibu chochote.

“Kwanza ni seme ninafuraha kujiunga na kocha wangu wa zamani japo kuwa leo (juzi) tumepoteza mechi dhidi ya timu yangu ya zamani lakini muda bado upo na Singida ni timu bora,” alisema Kaseke.

 

Ibrahim Mressy | Dar es Salaam

Leave A Reply